Search This Blog

Wednesday, April 17, 2013

UJUMBE WA FIFA WAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI LEO

 Mkuu wa Idara ya Uanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Primo Corvaro akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kumaliza kufanya mahojiano na baadhi ya wagombea walioenguliwa kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). (Picha na Habari Mseto Blog)

Primo Corvaro - '' Siwezi kusema kwamba ni sahihi au sio sahih , tumekuwa hapa kwa siku mbili na lazima tuendelee na kazi ya kukusanya taarifa mbali ambazo lazima tukae na kuzijadili kwa kushirikiana  na wenzetu wa idara ya sheria toka CAF na FIFA ili kuweza kupata undani wa  nini hasa kilitokea.
Unajua kuna uwezekano wa vitu vItatu kutokea , tunaweza kuamua mchakato uendelee pale ulipoishia , kwa maana ya kuyakubali  yale ambayo yalifanyika kabla ya ujio wa FIFA kuwa ni sahihi na tuendelee nayo,
tunaweza pia kuamua kuwa mchakato wa uchaguzi urudiwe upya,  au pia tunaweza kusema mchakato urudiwe kwa kuwahusisha wale ambao tayari walikuwa wameandikishwa tangu hapo awali , hivyo tunaweza kufanya lolote  kati ya hayo lakini kwasasa siko kwenye nafasi ya kusema kuwa tumefikia wapi ila ninachoweza kusema ni kwamba lazima matokeo yatapatikana hivi karibuni na tanzania itayafurahia.''

1 comment:

  1. Sasa FIFA itakapotoa maelekezo yake ninaomba waandishi wa habari na wachambuzi wa soka hasa wachezaji wa zamani itabidi tuheshimu maelekezo yatakayotolewa kwa ajili ya mustakabali wa soka la Tanzania badala ya kuanza tena kuupotosha umma wa watanzia na kutaka kuendeleza malumbano yasiyo na tija.Zimeanza juhudi za chini chini kupitia makala za magazetini kuwaandaa wadau kutokubaliana na uamuzi utakaotolewa na FIFA kwa visingizio vya kijinga kwamba FIFA isituamulie kiongozi wa TFF n.k.Tunaomba waandishi wa habari waheshimu taaluma yao badala ya kujali matumbo yao tu.

    ReplyDelete