Search This Blog

Monday, April 8, 2013

PAMOJA NA UONGOZI KUWARUDISHA KUNDINI MASTAA SIMBA - KOCHA LIEWING BADO AENDELEA KUMCHUNIA SUNZU

LICHA ya uongozi wa Simba kuwataka wachezaji waliosimamishwa kuanza mazoezi na wenzao baada ya kujieleza kwa maandishi, kocha Patrick Liewig bado ameonekana kumchunia Mzambia Felix Sunzu. Mfaransa huyo amekuwa akishikana mikono na baadhi ya wachezaji ambao wametoka kifungoni, lakini kwa Sunzu imekuwa tofauti kabisa. 

Kocha huyo alipohojiwa jijini Dar es Salaam baada ya mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Leader Club alisema kuwa kosa la Sunzu ni moja ambalo amekuwa hakubaliani nalo la kuondoka mazoezini bila taarifa. "Sina tatizo na Sunzu. Nafikiri wakati nawapa mikono, alikuwa mbali. Kwa hiyo sikuona kama ni lazima kumfuata." Mbali na hilo alisema; "Anatakiwa akubali majukumu ya timu. Lakini bado mahitaji athibitishe maandishi kwa uongozi na baada ya hapo, uongozi na mimi tutakaa kujadili suala lake kuona tutakubaliana vipi." 
Alieleza kuwa kosa la kwanza Sunzu alifanya walipokuwa kambini Zanzibar mashindano ya Mapinduzi aliondoka bila taarifa na la pili ni hili la kususia mazoezi Uwanja wa Etihad Mwananyamala ambao Simba ilikuwa ikiutumia kwa mazoezi yake.

9 comments:

  1. SIMBA WAMESHAANZA KUWEWESEKA NA KICHAPO TOKA KWA YANGA NDIO MAANA MARA WANAWAFUNGIA WACHEZAJI MARA WAWAAMBIE WAANDIKE BARUA ZA KUJIELEZA HOFU TUPU.MARA YA KWANZA WALIWAFUNGIA BOBAN NA NYOSO NA KUWATAKA WAJIELEZE NA HAWAKUFANYA HIVYO NA WAKASAMEHEWA,KICHAPO KIKO PALE PALE NA HUO NDIO UTAKUWA MWISHO WA RAGE

    ReplyDelete
  2. Uncle hapo juu huo sasa ni unazi, mtafute mwanajangwani mwenzio mjifariji mkiwa bado na deni la mkono! Mnyana ni mnyama usione kainama ukadhania paka.Karibuni tena dakika 90 za mahangaiko duniani hapo mtakapokutana uso kwa uso na mnyama raundi ya lala salama.Kwamba mnyama atatumia vijana ama wakongwe sio suala linalokuhusu!!!

    ReplyDelete
  3. Simba ichezeshe vijana au wakongwe bado timu yao yote ni mbovu,na kuna uwezekano wa kumaliza ligi nafasi ya tano.Baada ya matokeo mabovu eti itabadilika mechi ya mwisho na kuifunga Yanga kwa vile mwaka jana ilishinda 5 hizi ni ndoto za mchana.Mpira ungekuwa hivyo nadhani Azam wangeifunga Yanga MSIMU HUU kwa vile mmsimu uliopita walishinda mechi zote mbili dhidi ya Yanga.Kwa akili hizo ndio maana RAGE ATENDELEA KUWADANGANYA MILELE

    ReplyDelete
  4. nyie subirini tu siku ifike, yanga tumewaoa kanisani hatutawaacha mpaka kifo kitutenganishe. haijalishi kama tano tena kama moja, ila kipigo kwenu ni lazi ma kama kifo kwa binaadam. swhaini wakubwa nyie!!!

    ReplyDelete
  5. sasa mdau hapo juu,ubovu wa simba wewe unakuuma nini ndugu yangu? si usubiri kwanza muifunge ndio ulete habari zako za kinazi?

    ReplyDelete
  6. Wanayanga msimuogope sana Rage! Kuomba tumuondoe.Yeye hatocheza siku iyo hofu yenu ya nini? Cha muhimu mjipange kumkabili mnyama siku hiyo atakuja kivingine kabisa msije mkakumbushiwa kipigo cha mkono kilichopelekea kumtimua Mchunga!! Azam ni saizi yenu nyie, kivumbi cha maangamizi hakikwepeki.Ushindi wa tia maji tia maji wakati mwingine mpaka mzawadiwe tuta mwisho wake ni Mnyama.

    ReplyDelete
  7. Wajangwani wote mada yenu ni 5-0, Rage nini tena anahusikaje hapo?Hata Manji mkono umemuuma kila anapokuwa kwenye vikao vya yanga Hoja kuu ni 5-0.Kuwa bingwa sio issue kwa kuwa Simba na Yanga zimeshakuwa Bingwa mara kibao.Halafu kuna 6-0 zile za mwaka 1973.Mnyama mbaya jipangeni.

    ReplyDelete
  8. Wewe wacha kuwa na akili za kushikiwa utasemaje unaifunga Simba wakati mechi haijachezwa,Yanga acheni akili za kitoto yani matokeo haya yamewafanya hata msahau msimu uliopita mlikuwa vp na Simba walikuwa vp...Ila ningependa kuwakatisha tamaa kwa kuwaambia hata Simba wavurugane vp kumfunga goal 3 ni zoezi gumu sana,mnatakiwa kujuwa MASHABIKI mna wakati mgumu sana mnapojiona mpo fit alafu tunawapangia Vijana wajekuwa toa nishai,tena watoto watavyotaka sifa maana hadi Ferguson atakuwa ana wa-mingle..ndo hapo mtakapo ona Uturuki ni safari tu kama safari zingine mnazofanyaga Bagamoyo/Tanga....

    ReplyDelete
  9. Tofauti ya washabiki wa Yanga na Simba inaonekana iko kwenye kitu kimoja,UPEO WA KUFIKIRI.Inaonekana washabiki wa simba wanachanganywa na matokeo mabaya ya timu yao msimu huu ndani na nje ya uwanja.Kwa upande wa Yanga inaonekana wanachotaka ni kuifunga Simba tu hata iwe 1-0 na sio lazima kushinda 5-0 kwani pointi ni zile zile tatu(3).Kwa washabiki wa Simba wao inaonekana hata wakifungwa goli 1-0 na Yanga watafanya sherehe kwa sababu kwa akili zao kufungwa na Yanga ni lazima iwe 5-0.Hii ndio tofauti ya washabiki wa simba na yanga.

    ReplyDelete