Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka mshambuliaji Nsa Job wa
Coastal Union kuwasilisha maelezo yake juu ya madai kuwa alipewa rushwa
ya sh. milioni mbili ili asiifunge moja ya timu vigogo vya soka nchini.
Job
alikaririwa Aprili 3 mwaka huu na kituo cha redio cha Clouds FM katika
kipindi cha Amplifier kuwa alipewa kiasi hicho cha fedha na kiongozi wa
timu husika ili asiifunge katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, lakini
alipokea fedha hizo na kuifunga timu hiyo.
Baadaye
kiongozi huyo alikuwa akimtaka arejeshe fedha hizo. Pia TFF
imekiandikia kituo hicho cha redio kutaka nakala ya kipindi hicho ili
pamoja na maelezo ya mshambuliaji huyo vipelekwe katika Kamati ya
Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya Simba na Villa Squad mzunguko wa pili ligi kuu ya vodacom 2011/2012 na mhusika tayari ameachia ngazi simba sc
ReplyDeleteTFF THAT IS LACK OF PRECEDENCE.....WHAT ABOUT INVOLVING TO THE NATIONAL TEAM PLAYERS WHO WERE ACCUSED BY THEIR CLUB THAT THEY WERE INVOLVED IN CORRUPTION?
ReplyDeleteNsa naye inabidi apewe adhabu kwa nn amesubiri muda upite ndiyo azungumze?
ReplyDelete