KOCHA Mkuu wa Simba Patrick Liewig ameweka wazi mipango yake ya usajili kwa ajili
ya msimu ujao wa ligi na tayari amepanga kusajili wachezaji watano wapya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.
Mfaransa huyo alisema kuwa anaamini kuwa akitupa karata zake vyema kwenye usajili bila shaka Simba msimu ujao utakuwa vizuri.
“Msimu
ukimalizika nina mpango wa kusajili wachezaji watano ambao kwa kipindi
hichi nimewatazama na ninaona kuwa wanaendana na matakwa ya kikosi
changu kuanzia nidhamu hadi uwezo."
“Tumekaa na wenzangu wa benchi la
ufundi lakini bado hatuja hamua yupi wa kumchukua na kumwacha, kwani
kwa kawaida ni wachezaji wa kutazama zaidi kwa sababu ni suala ambalo
linahitaji utulivu mwingi na umakini wa hali ya juu."
“Nadhani kwa
mtazamo wangu na makubaliano na benchi la ufundi, naona kuwa tutasajili
watano ambapo kati yao wawili watakuwa ni wa nafasi ya ulinzi, kiungo
mmoja na washambuliaji wawili."
Kocha huyo amekuwa akieleza mara kwa mara kuwa anatarajia kubadilisha hali za wachezaji na kuwawezesha
kuonesha kiwango kizuri ili kulingana na dhamani ya pesa wanazochukua kwenye klabu hiyo.
“katika
usajili wangu, natarajia kuwachukua wachezaji wawili wa kimataifa,
wakati wengine watatu watakuwa ni wa hapa nyumbani Tanzania na
kushirikiana na yosso waliopo,” alisema kocha huyo.
Yosso waliotokea
Simba B ambao Liewig amekuwa akiwatumia kwenye michezo ya ligi ni pamoja
na mabeki Miraji Adam na Hassan Khatib, viungo Abdallah Seseme na Said
Ndemla na winga Haroun Athuman 'Chanongo' wakati upande wa ushambuliaji
ni Rashid Mkoko.
Wazoefu waliopo kwenye kikosi hicho ni Juma kaseja, Nassoro ‘Chollo’, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa na Shomari Kapombe.
No comments:
Post a Comment