Search This Blog

Monday, April 8, 2013

EXCLUSIVE: TAKUKURU YASHINDWA KUTHIBITISHA ERASTO, MORAD, DIDA NA AGGREY MORRIS KUPOKEA RUSHWA


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliyokuwa ikifanya uchunguzi wake dhidi ya wachezaji wanne wa Azam FC
waliotuhumiwa kupokea rushwa kupanga matokeo, imeshindwa kuthibitisha tuhuma hiyo.
Wachezaji ambao walikumbwa na kashfa hiyo ni kipa Deogratius Mushi 'Dida' na mabeki Erasto Nyoni, Said Morad na Aggrey Morris ambao wapo huru baada ya uchunguzi kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo.
Kosa la kupokea rushwa ni kinyume na Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.
Kwa mujibu wa kifungu hicho ni kosa kwa mtu yoyote kuomba, kupokea, kushawishi au kulazamisha kupewa rushwa au kuahidi kutoa rushwa.
Afisa Uhusiano wa TAKUKURU, Doreen Kapwani alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa
Wachezaji hao walituhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kupanga matokeo ya mechi kati ya Azam FC na Simba SC iliyochezwa Oktoba 27, mwaka jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Simba ilishinda mabao 3-1.
"Tuhuma hizo ziliwasilishwa TAKUKURU Mkoa wa Temeke Novemba 9, mwaka jana na Azam ikiwatuhumu wachezaji hao kupokea kiasi cha Sh7 milion kutoka kwa uongozi wa Simba wagawane na kupanga matokeo ya mechi hiyo."
Kapwani alisema fedha hizo zilidaiwa kupokelewa siku moja kabla ya mechi hiyo ambapo ni Oktoba 26, mwaka jana.
Pia, alieleza kuwa Azam imeweza kutimiza wajibu wake wa kushiriki katika kuzuia na kupambana na rushwa kwa kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU, chombo ambacho ndicho chenye dhamana na mamlaka ya kisheria kuchunguza makosa ya rushwa.
"Tunatoa wito kwa taasisi nyingine na wananchi kwa ujumla, kuendelea kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU ili kwa pamoja tuweze kudhibiti vitendo vya rushwa katika nchi yetu.

2 comments:

  1. Mnnh kazi kweli kweli!!! Kuna issue za kushushiana heshima na hadhi kwa waliotuhumiwa kutoa na kupokea iyo rushwa.Wadau na waungwana wajitokeze kutujuza au ndo mambo yameishia hapo? Kila mwenye kujisikia kumchafua mtu anajitangazia tu fulani mla/mtoa rushwa! Halafu majibu ya TAKUKURU "tumeshindwa kudhibitisha"Huu utakuwa mchezo wa kitoto! Mdau

    ReplyDelete
  2. Kule Mahakamani watataka evidence na kukidhi taratibu nyingine za kiufundi za kisheria(legal technicalities) ambazo ni vigumu kupata uthibitisho au kuzikidhi kwa kuzingatia mazingira ambayo rushwa zinatolewa katika mpira.Vyombo vya kiutawala vya mpira huwa havifungwi kwa kiasi kikubwa kukidhi taratibu hizo za kisheria ilimradi Mtuhumiwa amepewa haki ya kusikilizwa. Ushahidi wa mazingira UNAWEZA kupewa nafasi kubwa.Kwa mfano timu zinafungana mabao 10-10 KATIKA MECHI AMBAYO ZOTE ZINAHITAJI IDADI HIYO YA MABAO.Ukienda TAKUKURU watataka evidence lakini kimpira wataangalia matukio ya uwanjani kujiridhisha kuwepo au kutokuwepo kwa UPANGAJI WA MATOKEO.Kule England John Terry alishinda kesi ya ubaguzi wa rangi mahakamani lakini iliporudi kwenye vyombo vya kisoka alipatikana na hatia.Naishauri TFF nayo ifanye uchunguzi wake binafsi wa kisoka kujiridhisha na tukio hili na kulinda heshima ya mchezo huu wa kuvutia .Nyoni na Dida hawakucheza mechi ile ,Aggrey alicheza lakini awali hakuwa mmoja wa watuhumiwa,sasa wamehusikaje ni jambo linalohitaji uchunguzi wa kina na wa kimpira.

    ReplyDelete