Search This Blog
Monday, April 8, 2013
AZAM FC SASA KUPAMBANA NA TIMU YA JESHI LA MOROCCO
Na Baraka Mpenja ,Dar es Salaam
Mabingwa mara mbili wa kombe la mapinduzi na makamu bingwa wa kombe la Kagame, klabu ya Azam fc yenye makazi yake Mbande Chamaz Complex imefanikiwa kufuzu raundi ya tatu ya kombe la shirikisho licha ya kutoka suluhu pacha ya bila kufungana dhidi ya klabu ya Barrack Yc kutoka nchini Liberia.
Akizungumza na matandao huu muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa jana, afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema wamepokea vizuri matokeo ya mchezo huo ingawa hesabu zao zilikuwa kupata ushindi wa nyumbani.
“Mpira wakati Fulani hukataa, leo bahati haikuwa yetu kabisa, tumejaribu kutengeneza nafasi lakini hatukufanikiwa kufunga, wengi watajiuliza sana, kila mtu akumbuke kuwa wachezaji walioshindwa kufunga leo, ndio wale waliofunga mabao mawili kule Monrovia nchini Liberia”. Alisema Idd.
Idd alisema ushindi wa ugenini wa 2-1 umewafanya wasonge mbele ingawa Barrack Yc walikuwa wanahitaji ushindi kama walivyofanya kwao, lakini wamekumbana na kisiki cha mpingo leo uwanja wa taifa.
“Baada ya mchezo huo, kocha wetu mwiingereza Sterwart Jan Hall ameridhika na matokeo, kilichobaki na kuangalia hesabu za ligi kuu soka Tanzania bara kabla ya kuanza kuwaangalia wapinzani wetu siku zijazo”. Alisisitiza Idd.
Pia alisema kuwa watanzania wengi walidhani timu ya Barrack Yc ni nyepesi baasa ya kuwafungwa kwao, lakini kiukweli ni timu ambayo imejipanga vizuri na ndio maana leo imewatoa jasho uwanja wa taifa baada ya kutoka nao 0-0.
“Unajua leo kila timu ilakaza kupata matokeo ya ushindi, tulishambuliana kwa zamu, lakini kwa upande wetu washambuliaji wetu kama John Bocco, Kipre Herman Tchetche walikosa nafasi za kufunga, yote kwa yote ni mchezo wa soka bwana”. Alisema Idd.
Afisa habari huyo aliongeza kuwa baada ya matokeo ya leo, sasa wanajipanga kukutana na timu ya jeshi la Morroco, kutokea kaskazini mwa bara la Afrika, FAR Rabat ambao ni wagumu kushindwa.
Katika mchezo huo wa kukata na shoka, kikosi cha wana lambalamba Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, Joackins Atudo, David Mwantika, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’, Humphrey Mieno/Abdi Kassim na Brian Umony/Khamis Mcha ‘Vialli’.
Barack Y.C ya Liberia mashine zao zilizoanza zilikuwa.; Winston Sayouah, Karleo Anderson, Joseph Broh/Prince Kennedy, Cammue Tummomie, Prince Jetoh, Junior Barshall, Benjamin Gbamy, Abraham Andrews, Randy Dukuly/Erastus Wee, Mark Paye na Ezekiel Doe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Azam bado wana matatizo makubwa upande wa ulinzi na hivo wanatakiwa kufanya marekebisho makubwa kabla ya hatua inayofuata.Jockins Atudo ni mzuri zaidi anapocheza beki wa pembeni kulia na alipokuwa Tusker alisaidia sana timu kwenye kulinda,kuunganisha timu na kushambulia.Combination ya Mwantika na Atudo beki ya kati bado siyo nzuri sana.Aidha pembeni nako Himid Mao na Waziri Salum bado wana mapungufu ya kiufundi ambayo wamorocco wanaweza kuyatumia kupata bao la mapema na kuwachanganya Azam.
ReplyDelete