Search This Blog
Monday, April 8, 2013
MUSSA MGOSI: JKT TUTAPAMBANA TUBAKI LIGI KUU
Na Baraka Mpenja Dar es Salaam
Mchezaji nguli wa maafande wa JKT Ruvu, pia aliyewahi kutamba akiwa na wekundu wa Msimbazi Simba, DC Mote Mapembe ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pamoja na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars, Musa Hassan Mgosi ametamba kuiokoa klabu yake isishuke daraja msimu huu.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na matandao huu, Mgosi ambaye jina lake ni la kibantu likimaanisha mwanaume, amesema kamwe timu yake haiwezi kushuka daraja kufuatia hali yake kuimarika na kurudi katika kiwango chake cha kawaida.
“Nilikuwa majeruhi, lakini siku nne zilizopita nimeanza programu ya mazoezi, najiona kuwa makini, kilichobaki ni vita ya kukwepa panga la kushuka daraja, na kwa pamoja tutaweza”. Alisema Mgosi.
Nyota huyo ambaye jina lake haliwezi kusahaulika kwa wana Msimbazi kutokana na kufunga magoli muhimu, aliongeza kuwa ligi ya sasa ina ushindani mkubwa sana huku kila timu inaonekana kuwa imara zaidi inapocheza mechi.
Mgosi aliongeza kuwa yeye ni mchezaji wa kimataifa na ana uzoefu mkubwa wa kufunga magoli, hivyo lazima aibebe JKT Ruvu msimu huu ikiwa ni sehemu ya kuilipa fadhila timu hiyo aliyoanza nayo katika safari yake ya soka.
“Unajua JKT Ruvu ni nyumbani, wengi walijiuliza kwanini nimeichagua nilipotokea Kongo, kikubwa timu hii ni nyumabi kwangu, nilianzia soka hapa, nimerejea kuinusuru na lazima ibaki ligi kuu”. Alisema Mgosi kwa kujiamini.
Akizungumzia ndoto zake za kurudi timu ya taifa kwa mara nyingine, Mgosi alisema yeye ni mchezaji mwenye imani mkubwa na nidhamu kubwa ya mazoezi, hivyo ataweza kurudi tena timu ya taifa inayonolewa na kocha Kim Paulsen.
Mgosi alisisitiza kuwa timu ya taifa ya sasa ina wachezaji wazuri, wanapata huduma zote kutoka kwa wadhamini, hivyo anatamani kurudi ili alitumikie taifa kwa moyo wote.
Maafande wa JKT Ruvu wapo hatarini kuaga michuano ya ligi kuu, kwani mpaka sasa wamejikusanyia pointi 22 wakiwa nafasi ya 10 kati ya timu 14 za ligi hiyo.
Jumatano ya Aprili 10 watakuwa ugenini katika dimba la CCM Mkwakwani Mkoani Tanga “waja leo waondoka leo” kumenyana na wagosi wa kaya Coastal union.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment