HATIMAYE Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro
imeikabidhi Timu ya Taifa(Taifa Stars)basi jipya la kisasa lenye thamani
ya Sh 200 litakalotumika kwa safari za timu hiyo.
Hafla ya
makabidhiano hayo ilifanyika makao makuu wa TBL jijini Dar es Salaam
jana na kuhudhuriwa na maofisa wa ngazi za juu wa TFFna baadhi ya wadau
wa soka.
TBL ilikabidhi basi hilo kama sehemu ya utekelezaji
wa udhamini wake kwa timu hiyo ulioingiwa Mei mwaka jana kati yake ya
Shirikisho la Soka Tanzani(TFF).
Akizungumza wakati wa hafla
hiyo,Meneja wa Bia Kilimanjaro,George Kavishe alisema kuwa basi hilo
kutoka kampuni ya Yutong limezingatia vigezo kwa matumizi ya timu ya
taifa.
"Wachezaji wetu lazima wawe na nafasi nzuri ya kupumzika
wakati wa safari ,na hiyo ndiyo sababu iliyotufanya tununue basi hili la
kisasa,tunaomba
mlitunze,".alisema Kavishe.
Kwa upande wake Rais wa TFF,Leodegar
Tenga aliishukuru TBL kwa kukabidhi basi hilo na kusema shirikisho lake
litaendeleza kutekeleza yale yote yaliyomo katika mkataba baina ya
pande hizo mbili.
"Ahadi yangu ni kwamba TFF itaendelea
kushirikiano nanyi sambamba na kutekeleza yake yote yaliyomo katika
mkataba baina yetu,".alisema Tenga.
No comments:
Post a Comment