Mmiliki wa AC Milan Silvio Berlusconi amesema matamanio yake ni kuifanya klabu hiyo iendelee kuwa chini ya familia yake, lakini amekiri hali inaweza kubadilika kutokana na hali ya mbaya kiuchumi ya Italia.
Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Italia amkeuwa akiiongoza klabu hiyo ya Serie A tangu 1986 na uongozi wake umeifanya Milan kuwa moja ya vilabu tajiri barani ulaya. Japokuwa, hali imebadilika miaka ya hivi karibuni huku maofisa wa juu wa klabu wakisema kwamba msimu huu ni muhimu na lazima kuwa na mipango sahihi ya kiuchumi.
“Ningependa kuendelea kuifanya Milan kitu cha familia yangu." Berlusconi aliliambia shirika la habari la Italia ANSA. “Bado nakumbuka wakati baba yangu aliponichukua kwenda uwanjani na sikulipia tiketi kwa sababu nilikuwa mdogo sana. Klabu hii ni sehemu ya familia. Mtoto wangu Barbara sasa hivi ni sehemu ya kampuni, na ningependa kuendeleza jambo hilo. Kwangu mimi, Milan ipo moyoni mwangu. Kwa miaka mingi tumetumia fedha nyingi nyingi sana, inawezekana nyingi mno."
Milan imekuwa ikihusishwa na kununuliwa katika kipindi cha miezi kadhaa na Berlusconi amekubali kwamba wanaweza kufungua uwezekano wa kuingiza mwekezaji. "Japokuwa kupenda kwangu hii timu iendelee kuwa chini ya familia, haimanishi kamba nafunga uwezekano wa kuingiza mwekezaji. Ikiwa hali ya uchumi itaendelea kuwa hivi ilivyo sasa, mabo yanaweza yakabadilika. Kuingiza fedha kutoka nje ndani ya Milan? Labda ikinibidi kufanya hivyo."
No comments:
Post a Comment