Mwaka wa kalenda sio sawa na msimu wa soka , pamoja na hilo hakuna pingamizi juu ya uwezo wa Lionel Messi ambaye jana amepewa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara yake ya nne mfululizo moja ya sababu za kumpa tuzo hiyo ikiwa mabao 91 aliyofunga katika miezi 12 ya mwaka uliopita .
Bila ubishi wowote tunashuhudia kitu maalum katika mchezo wa soka nacho ni Lionel Messi . Hata hivyo wakati tuzo , mabao na sifa zikiendelea kumwagika kwa Messi , lazima tujiulize kitu kimoja haya yote yanasababisha madhara ya aina moja au nyingine kwa timu yake ? Makala hii itatazama mwenendo wa kutia hofu kwa mashabiki wa Barca mwenendo unaoonyesha jinsi Barcelona inavyokuwa tegemezi sana kwa Messi tofauti na Messi kuwa na msaada mkubwa kwa timu yake. Messi ana miaka 25 na ametwaa mataji yote kwa upande wa klabu katika kipindi kifupi cha maisha yake kama mchezaji wa Barcelona .
Uwezo wake umebadilisha mchezo wa soka ,movement zake uwanjani,maamuzi,kiwango cha mambo anayofanya akiwa na mpira mguuni kwake na uwezo wake mkubwa wa kumaliza akiwa kwenye eneo la hatari kwa ujumla vyote hivi vimefanya makocha na wachezaji wengi kujaribu kubadilisha uchezaji wa timu zao kuwa kama wa Messi.
Kipaji na uwezo wake vimeipa Barcelona mtindo na mfumo mzima wa soka linaloonekana Camp Nou. Messi ana uwezo wa kuamua matokeo ya michezo kwa uwezo wake mwenyewe pasipo kutumia nguvu nyingi tofauti na wachezaji wengi. Kama tuzo ya Ballon D'or ni utambulisho wa mchezaji bora kwa uwezo binafsi basi Messi anastahili kupewa tuzo hii kwa mara nyingine. Hata hivyo haya yote yanakuja kwa gharama ya mafanikio ya timu ya Barcelona
Mwaka mtupu kwa Barcelona.
Swali la kujiuliza ni moja , je huu umekuwa mwaka wa mafanikio kwa Messi . Hakuna ubishi katika hilo , Tuzo ya Ballon D'or inadhihirisha kuwa ulikuwa mwaka wake , hata hivyo pamoja na mwaka huu kuwa wake hali ilikuwaje kwa Barcelona kama timu? Jibu ni moja haukuwa mwaka mzuri kwa Barca kama timu tangu Pep Guardiola alipokuwa kocha wa timu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2008.
Hivyo basi kama Messi ni bora kiasi hicho , kama anaweza kufunga mabao 91 kwa klabu na timu ya taifa kwanini haukuwa mwaka wa mafanikio kwa Barcelona ? Sio kila sababu ya mwaka mtupu wa Barcelona inamuelekea Lionel Messi, Tukumbuke kuwa Barcelona ilitambulisha mtindo na mfumo mpya na Kocha Pep Guardiola ambaye huenda alichangia kwa kuwatumia wachezaji vijana kina Isaac Cuenca na Christian Tello kuliko kiasi, labda sababu ilikuwa majeraha kwa watu kama David Villa,Puyol na Iniesta ambao waliumia kwa vipindi virefu na tofauti.
Sababu nyingine yaweza kuwa kushuka kwa viwango vya wachezaji kama Gerald Pique na Pedro pamoja na kusajiliwa kwa Cesc Fabregas ambaye pamoja na kufundishwa soka la Barcelona alirejea Nou Camp akiwa mchezaji tofauti na yule aliyeondoka akiwa na miaka 16 huku akiwa na falsafa tofauti kidogo ya Kiingereza zaidi kwenye soka lake. Alexis Sanchez pia hakuwa yule aliyetarajiwa, haya yote yalisababisha Barcelona kumtegemea sana Lionel Messi. Kwa kifupi haukuwa msimu mzuri kwa Pep Guardiola . Baada ya kuwa na msimu mzuri kwa miaka ya 2010-2011, Guardiola aliona haja ya kubadilisha mtindo wa kikosi chake.
Maamuzi mabaya na majeraha kwa wachezaji wenzie yalisababisha Messi kutegemewa kuliko kawaida kuiokoa Barcelona. Guardiola alilazimika kupoteza falsafa yake ya kujenga timu inayochangiwa na walau kila mchezaji na matokeo yake alimpa nguvu nyingi Messi kuliko wachezaji wengine. Mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2011/2012 mpango wa Barcelona ulikuwa kutwaa taji la dunia kwa vilabu na kutetea ubingwa wa Ulaya . Nusu fainali ya Ligi ya mabingwa dhidi ya Chelsea ndio ilionyesha udhaifu wa Barcelona wa kumtegemea sana Messi na jinsi timu ilivyokosa Balance.
Kwa kifupi Barcelona ilikuwa na kundi la viungo ambao kazi yao ilikuwa kumpa Messi mipira kwenye maeneo ya hatari. Mawinga Villa na Pedro ambao misimu ya awali walikuwa muhimu sana hawakuwepo. Messi alikosa sumu yake na alikuwa mwepesi kucheza dhidi yake kwa kuwa alilazimika kushuka chini kutafuta mipira kuliko kawaida, na beki ya Chelsea haikuwa na hofu kwa kuwa kwa kuwa Penetration ya Barcelona haikuwepo na hata pale ilipokuwepo haikumkuta Messi akiwa eneo la hatari hivyo Chelsea hawakuwa na sababu ya kuwa na hofu. Safu ya ushambuliaji ya Barca ilikuwa inatabirika na ilikuwa nyepesi kukabika na ndio maana Barcelona walihangaika kuivunja defence ngumu ya Chelsea ambayo ilitambua mapungufu haya ya Barca na kuyafanyia kazi kikamilifu, hata presha kubwa kisaikolojia kwa Messi katika mechi hizi mbili ilikuwa dhahiri.
ITAENDELEA.......
Mimi nadhani si haki Messi kupewa tuzo kwa sababu kadhaa.Kwanza katika semi finalist watatu wawili wanatoka Barca na wote ndiyo walioflop 2012,mmoja ametoka Madridambaye ni Ronaldo aliyeshinda La liga. Messi ametamba na Barca pekee.hatujui itakuwaje kama siku akienda kucheza Ujerumaini au Ufaransa iwapo atamudu.Sasa iwapo alichezea Barca tu na halafu akaflop hii ilikuwa ni picha ya kuonyesha hastahili kuwa mchezaji bora wa Dunia kwa sababu anachezea culture ya Barca ndiyo maana hata akienda timu ya taifa;Argentina Messi hang'ai kwa sababu Argentina hawachezei kwa culture ya Barca hali inayompa taabu sana Messi. Na hata jana jana aliposhinda kwa ngekewa ameeleza masikitiko yake hayo kushindwa kutamba na Argentina.Tatizo ninaloainishia udhaifui wa Messi ni hili, toka ana miaka 13 alisajiliwa na akawa anachezea Barca tu hajatoka kuwa exposed nje ya Barca achilia mbali Spain. Kwa hiyo hawezi kuwa mchezaji bora wa Dunia.Dunia si Barca.Ronaldo surely Is kwa sababu katamba Ureno,Uingereza na sasa Spain,ligi tatu tofauti na timu tatu tofauti na kila anakokwenda kiwango kinaongezeka kuliko alikotoka. wakati Messi akienda Argentina tu ana flop!Nitapingana naye kwa hilo tu. Iko walakini labda watu wako posessed na Messimonia bila kuzingatia fact hizi.Pia Ronaldo ni winger (midfielder)anafunga goli zaidi ya 40 kwaligi mbili kubwa tofauti duniani; hiyo peke yake ni credit tafuta winga duniani mwenye idadi hiyo hakuna kwa ligi zote.Kwa Messi kufunga goli hata 200 ni sawa kwa kuwa si ndiyo kazi ya striker? Ingekuwa Varmellen amefunga magoli hayo yote anbvaye ni beki kila mtu angempa tuzo kwa kuwa ni ajabu beki kufunga magoli,sasa Messi amefanya nini cha ajabu?
ReplyDeleteNaamini pia ht ww una mapungufu katika vision yako katika soka, unaposema messi ana shine ktk barca tu kama ndio kigezo kwann pia usiseme INIESTA alistahili simply bz kashinda everything ukilinganisha na ronaldo n messi? kashinda Euro, Kashinda "HESHIMA YA DUNIA" world cup n kashinda mabala, kama ndio kigezo basi anastahili yy. Lakini tukirudi ktk ukweli soka la sasa linakosa watu kama messi kwasababu, vtu anavyo onesha messi vinafanya watu turudi ktkt kitu kinacho itwa "NATURAL FOOTBALL", `players are born n not created` kama ligi yenu ya uingeleza ilivyo jaa made players. so unapokuja kwa messi, alistahili kwa sababu amezaliwa na uniqueness nyingi ambazo kama yangekuwa mamuzi yangu, angepigiwa kura aingie kenye record za "MAAJABU SABA YA DUNIA". Its GOD gift to football to have MESSI,so lets proud to have him.
Deleteduh,hamumpendi messi nyinyi!!!!!DOGO ana kipaji acheni longolongo,wale waliompa kura zao wanaujua mpira kuliko nyinyi,najua nyie mlitaka saaaaana apate christiano ronaldo....eti sababu real madrid walichukua la liga,basi kwanini asingepewa aguero basi kwa sababu naye man city ilichukua premier,au mzee pirlo aliyekuwa anaichezesha juve anavyojisikia yeye?
ReplyDeletenaungana na wachangiaji wawili wa mwisho kuwa messi alistahili tena bila ya shaka lolote.nadhani mchangiaji wa kwanza ana mapungufu ya kuujua mchezo wa soka kama alivyoeleza mchangiaji wa pili hapo juu.kinachonishangaza zaidi kuhusu uelewa wake mchangiaji wa kwanza ni pale anaposema ili uwe mchezji bora wa dunia ni lazima ucheze ligi tofauti au uame timu. huu ni upotoshaji mkubwa na ufinyu wa mawazo kwani lazima atambue kuwa anaposema messi anashaini kwenye timu moja na ligi moja kwanini asijiulize hiyo timu moja ndiyo inayozinyanyasa timu nyingi za ulaya na dunia hivyo kuchukua ubingwa.maana yake hiyo timu nibora.ligi anayoiita pengine ni nyepesi kwa mawazo yake juzi ndiyo imetoa wachezaji wote 11 bora wa mwaka. hakuna hata mchezaji hata mmoja wa ligi yake anayoona messi anastshili kujipima.je huo sio uwezo mdogo wa muono?na anamgang'aniza messi ahame Barcelona, hivi nani ajui kwasasa Barca ni timu bora? Nani angependa kutoka peponi kuhamia jehanamu? waliopiga kura sio wachezaji wa Barca wala Argentina, ni macaptain na makocha wanaolijua soka kuliko yeye.
ReplyDeletenadhani tuzo hiyo kapewa kama mchezaji mwenye kipaji kikubwa kwa sasa lakini tukizungumzia mchezaji bora tunalenga sehemu nyingi kama vile mchango wa mchezaji kwenye timu aliyopo kwa wakati huo...ukizungumzia eti messi kavunja eakodi ya magoli mengi kwenye mwaka mmoja kidogo nina mawazo tofauti. Rekodi hiyo inapimwa kwa ulinganisho wa magoli na siyo idadi ya mechi hawa watu walizocheza. Messi alifikisha magoli kama ya Muller baada ya kucheza mechi 4 zaidi kama sijakosea. Huko ndio kuvunja rekodi? labda tungealia wastani wa magoli kwa kila mechi ingekuwa bora zaidi kuliko ujumla wa magoli yote. Kama rekodi ni kigezo cha mchezaji bora wa dunia hebu jaribu kupitia rekodi za kila mchezaji utakuja kutambua kwamba wapo ambao wana rekodi zaidi ya huyo mchezaji bora.
ReplyDelete