Timu ya Young Africans Sports Club kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uturuki katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika katika uwanja wa Selen Football -Kalimya Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.
Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu hiyo la Denizlispor FC ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka jana na hivi sasa inapamabana kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
Baada ya kuwa na wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini Bielefeld ya ujerumani mwishoni mwa wiki itakua ni fursa nyingine nzuri ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu nyingine, hii itanisadia kuona maendeleo ya kikosi changu kutokana na mazoezi ambayo tumekuwa tukiyafanya tangu tulipofika alisema 'Brandts'
Denizlispor FC ni miongoni mwa timu zaidi ya 200 kutoka shemu tofauti duniani ambazo zimeweka kambi katika mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji wa zamani wa Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na Ivernes ya Uholanzi, mtanzania mzaliwa wa Uingereza Eric Odhiambo ni miongoni mwa washambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC.
Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen Football - Kalimya complex pemebeni kidogo ya mji wa Antalya.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Athumani Idd 'Chuji' na Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya Amrnini Bielefeld wanaendelea vizrui kabisa kwani wanaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine waliopo na timu mjini Antalya.
Kuhusu hali ya hewa leo haijaonekana kuwa tatizo kwa wachezaji kwani wanaonekana kuimudu na mda mwingi kwa sasa kumekua na jua linalowaka kuanzia asubuhu wakati wa mazoezi mpaka mida ya jioni, kwa leo hali ya hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyo hali ya hewa ni nzuri kabisa na jua linawaka mda wote.
yanga mmeonesha mfano mkubwa katika timu zetu za kitanzania... hongereni sana... wapo wanaokaa hawana kazi na kusema kwamba yanga inacheza na timu za daraja la tatu au la nne... Jamani watanzania tuacheni majungu na tuoneshe ushirikiano pale timu zetu zinapoonesha hatua ya kutaka kujiendeleza... safi sana Yanga Fc
ReplyDeleteYANGA BANA YAN MNACHEZA LIG KWENYE JOTO KAL 30 CENTIGREDI THEN MNAENDA MAZOEZ KWENYE NCH YENYE 4 CENTGREDI......HAYA BANA MI MGEN NCHI HII
ReplyDelete