SEHEMU YA 3
Jana katika mazungumzo yetu na kijana Juma Omary tuliishia katika sehemu anaelezea namna alivyofika jijini Dar es Salaam kwa miguu kutoka Morogoro. Leo tunaendelea katika sehemu ya tatu ambapo Juma anaelezea kiundani safari yake ya kuja kwa miguu Dar huku akiomba usaidizi kutoka kwa wahisani watakaoweza kumsaidia aweze kutimiza ndoto yake ya kucheza soka la kulipwa.................................
Suala la kutembea kwa miguu kutoka Moro mpaka Dar kidogo lilinistua na kunifanya nihisi Juma ananiongopea ikabidi nimdadisi aliweza vipi kufika Dar kutoka Moro, Je alikuwa anapajua kabla, kama sio ni nani alimuelekeza na kwa mujibu wake hakuwa na hata shilingi, je aliimudu vipi njaa na safari hiyo ya takribani siku mbili barabarani mpaka alipofika Dar?
Juma alinijibu: "Ni kweli haikuwa rahisi kwangu kufika Dar kwa kuwa nilikuwa mgeni. Hivyo njia niliyotumia na kuulizia watu tofauti na kuyafuata magari yaliyokuwa yanaelekea Dar. Kama nilivyosema mwanzoni nilitoka Mpanda na shilingi 25,000 na zote nilizitumia kwa kulipa nauli pamoja faini niliyopigwa kwenye treni hiyo, lakini kwa bahati nzuri kwenye treni pia nilikuwa na baadhi ya rafiki zangu ambao wenyewe walikuwa na safari tofauti na mie. Mmoja alikuwa akienda Shinyanga na mwingine alishuka Dodoma - hawa ndio walionisadia kwenye masuala ya misosi mpaka pale safari zao zilipoishia. Hivyo mpaka nafika Morogoro atleast nilikuwa tayari nimekula njiani kwa chakula alichonisaidia rafiki yangu aliyeshukia Dodoma. Treni iliwasili Moro asubuhi nikashushwa na kisha nikaanza safari yangu ya kuja Dar kwa miguu. Muda mwingine nilikuwa nakimbia taratibu na nilipochoka nilitembea kawaida. Nilitembea kwa muda mrefu mpaka inatimia saa 1 usiku nilikuwa nimefika eneo ambalo wenyeji walikuwa wakiliita Chalinze. Hapo nikalala nikiwa sijatia chochote tumboni zaidi ya kusaidiwa maji ya kunywa tu. Kesho yake alfajiri nikaanza tena kutembea kuja Dar na kwa uwezo wa mwenyezi mungu nikaingia hapa mjini kwenye mida ya saa 10 jioni, nikaulizia na nikaelekezwa pale kwenye klabu ya Simba."
Shaffih: Jambo la kutoka Moro mpaka Dar sio jepesi hata kidogo, tena hasa ukiwa njaa pia mgeni kabisa katika maeneo uliyopita. Umepitia changamoto na shida nyingi mpaka kufika hapa ulipo, Je ni nini hasa kilichokuwa kinasukuma na kukufanya usikate tamaa ya kufika Dar?
"Ni kweli nilikutana na changamoto nyingi, lakini nilipiga moyo konde na kuendelea na safari mpaka nilipofika hapa. Lengo langu kwenye maisha kwa sasa ni kuufanya mchezo wa soka kuwa ajira yangu rasmi. Nashukuru mungu nilifika Dar salama na hapa ndipo sasa nahitaji msaada wa wadau wanisaidie niweze kutimiza ndoto yangu," aliomba Juma Omary.
"Soka ni kitu ambacho nakipenda na nimebarikiwa kuujua mchezo wenyewe. Huko nilipotoka shule nilikuwa ni mchezaji ninafanya vizuri uwanjani na nilifanikiwa kutajwa kuwa mchezaji bora kwenye mashindano mbalimbali. Naamini nikisaidiwa kupata nafasi naweza nikathibitisha niyasemayo, na nitacheza kwa bidii ili kuifanikisha ndoto na kuwaridhisha watakanisaidia."
dogo aseme tu anahtaji msaada asaaidiwe sio kwamba alitembea kwa mguu kutoka moro mpaka kariakoo tena kwa sku mbili na hajala sio rahisi kama anavyofikiria yeye asesme tu ukweli atasaidiwa
ReplyDeletemuulize aliwezaje kutoka steshen morogoro mpaka barabara inayokuja dar huku mgen na kisha kutoka mbez mpaka kariakoo
We uliyetoa maoni hapo juu hujui shida na nahisi wewe ni HOTPOT FAMILY, si jambo gumu kama kweli unashida ya maisha na huenda mungu kamuonesha njia yake ya kutokea ni hii ya kuja Dar kusaka maisha kupitia Soccer. Kama Ismail Rage unasoma safu hii tafadhali mchukueni huyo dogo mfanyieni majaribio aingizwe Kikosi cha kwani ndiyo pekee hapa Tanzania yenye nia ya kweli ya kukuza soka la vijana na ili iwe njia moja wapo ya kumsaidia kijana huyo. Au Shaffih kama mdau mkubwa wa soka hapa TZ mtafute Rage na viongozi wengine wa Simba SC wamsaidie huyo kijana kukuza kipaji chake.
ReplyDeleteBy MKINGA C.J Mdau wa Soccer(KIMARA RESORT DSM)
Mimi naungana na mchangiji wa pili kwa sababu mchangiaji wa kwanza amezaliwa kwenye raha hawezi kujua shida ndio maana asema kwa haiwezekani kutembea kwa miguu kutoka moro mpaka dar ila angepitia maisha kama haya asinge changia kama hivyo.wito wangu kwa wadau wa soka wamsaidie huyu dogo wamfikishe kwa viongozi wa simba ili wamsaidie kijana huyu na yeye atimize ndoto yake ya maisha ya soka.sina la zaidi.
ReplyDeletedah!!! sina la kusema laiti ingekua njia panda, hata nauli ningekuchangia mi nilale njaa uende (azam) hawa wengine wababaishaji. big up bwana mdogo
ReplyDelete