Klabu ya Young Africans Sports Club itashuka dimbani siku ya
jumatano (Boxing Day) kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Tusker FC ya
nchini Kenya, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Akiongea na waandishi wa habari Afisa Habari wa Yanga
Baraka Kizuguto amesema Kocha wa Yanga anatarajiwa kuwatumia wachezaji
wake wote katika mchezo huo ambapo Yanga itatumia nafasi hiyo kuwatumia
karibu wachezaji wake wote ambapo timu hiyo inajiandaa kwa maandalizi ya
safari ya kuelekea nchini Uturuki kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa
ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
Mchezo huo utakua
mchezo wa kwanza kwa Yanga tangu ligi iliposimama mwezi novemba baada
ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi Kuu ya Vodacom, hivyo
itakua ni fursa kwa wanachama kuona timu yao ambayo ilianza mazoezi
tangu tarehe 26 Novemba kujiandaa na mashindano mbali mbali aliesema
"Kizuguto"
Pili itakua ni zawadi ya sikuuu ya
X-Mass kwa wapenzi, wanachama na washabiki wa soka nchini, ambapo
wapenda soka nchini watatumia fursa hiyo kusherekea sikukuu kwa kutazama
soka safi ambalo hawajaliona kwa kipindi kirefu.
Tatu
utakua ni mchezo wa mwisho katika kufunga mwaka kabla ya kusafiri
kuelekea nchini Uturuki, pia ikitumia mchezo huo kuwaaga wapenzi,
washabiki na wanachama wake kabla ya safari hiyo ya kambi ya mafunzo
itakayochukua ya takribani wiki 2.
Aidha
Kizuguto ametangaza Viingilio vya mchezo huo kuwa ni Tsh 15,000/= VIP A,
Tsh 10,000/= VIP B, Tshs 7,000/= VIP C, na Tsh 5,000/= kwa Orange, Blue
na Green.
Kwa upande wa waandaji wa mchezo
huo, George Wakuganda amesema mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya
Yanga na kwamba Yanga itatoa zawadi kwa mashabiki wake
source:http://www.youngafricans.co.tz
ACHENI TAMAA VIINGILIO VIKUBWA,KIINGILIO CHA CHINI WEKENI 3,000 ILI MPATE PESA NYINGI ZAIDI
ReplyDeleteAcha kuongea mbwembwe unaijua Yanga wewe,Timu kubwa kuliko zote nchini,unataka kiingilo chake kiwe sawa na Simba? Umuone Niyonzima,kabange Twite,Mbuyu Twite kwa sh.3000 haitakuwa Yanga itakuwa toto au simba.
ReplyDeleteKweli January na kama anataka kujua Yanga kweli inapendwa aende kesho Taifa aone umati huo regardless ukubwa wa kiingilio.YANGAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
ReplyDelete