Search This Blog
Thursday, October 11, 2012
UDHAMINI WA KAMPUNI YA MIKOPO KUWAKIMBIZA DEMBA BA, CISSE, TIOTE NA BEN ARFA NEWCASTLE??
Kumekuwepo na hisia kwamba Newcastle inaweza kuwapoteza wachezaji wake wenye imani kali ya dini ya kiislamu kama Demba Ba, Papiss Cisse, Cheik Tiote na Hatem Ben Arfa baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa jezi ambao unaweza ukawa unakinzana na sheria za dini ya kiislam.
Newcastle wametangaza jana kwamba klabu hiyo imekamilisha dili la mamilioni ya fedha na kampuni ya mikopo ya Wonga, ingawa kumekuwepo na mawazo kwamba Ba, Cisse, Tiote na Ben Arfa wanaweza kukataa kuvaa jezi yenye logo ya kampuni hiyo inayopata faida kutokana na biashara ya kuazima fedha huku wakirudishiwa fedha hizo kwa riba - kitendo ambacho ni kinyume sheria za dini ya kiislamu, kwa maana hiyo wanaweza hata kuondoka ili kuepeukana na dhambi hiyo.
Siku za nyuma mchezaji Freddie Kanoute aligoma kuvaa jezi za Seville zilizokuwa na udhamini wa kampuni ya kamari ya 888.com kifuani. Kanoute mwishowe aliruhusiwa kuvaa jezi siyokuwa na mdhamini lakini akakubali kuvaa jezi yenye logo ya mdhamini wakati wa mazoezi akiwa na maana ya kutoitangaza kampuni hiyo kwa mashabiki wake na waklabu kiujumla.
Swali linabakia je Newcastle watakuwa tayari kuwapoteza wachezaji wao wanne muhimu au watakubalia kuwatengenezea jezi ambazo zitakuwa bila na nembo ya mdhamini mpya? Muda pekee ndio utatoa majibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment