Siku chache baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba waziri wa michezo na utamaduni ataunda tume ya kuchunguza TOC, mwanaharakati na mkimbiaji Willlheim Gidabudayi ameibuka na kumuomba waziri asijaribu kuunda tume hiyo kabla kupitia ripoti ya Olimiki kutoka kwa vyama vvya michezo husika kabla ya kuunda tume huru ya kuchunguza TOC kufuatia madai ya ufisadi ambao wadau kama akina Gidabudayi wumetoa sambamba na ushahidi unaoridhisha kama ambavyo ameandika hapo chini:
1). Ni kwa nini waziri asiunde tume ya kuchunguza madai ya DOLA ZA INDIA?, au wizarani pia waliitafuna dola hizo za India?. Dola 100,000 ni takriban TSH: 160,000,000/= ni ajabu sana serikali kudhani kwamba si lolote la kuchunguzwa!!.
2). Pia ni kwa nini hadi leo waziri hajawahoji TOC kuhusu matumizi ya USD 100,000 sawa na TSH: 160,000/= ambazo TOC walidai kuzitumia kwa maandalizi ya kwenda London. TOC walitoa matumizi yao kwa vyombo vya habari lakini matumizi yale yalijaa uongo ambao sisi wadau tunayo ushahidi. Je waziri anadai vipi ripoti ya Olimpiki kabla ya kuchunguza ufisadi ndani ya TOC na baadhi ya maofisa wakubwa wa wizara yake?.
3). Je ni kwa nini hadi leo waziri hajaagiza kupatiwa idadi kamili ya fedha zilizotolewa na Olympic Solidarity yaani "quadrennial financial aid" kuanzia 2009 hadi 2012?. Sisi wadau tumeonyesha kutoridhika na kiasi kikubwa kutumiwa na vigogo wa TOC kujinufaisha wenyewe kwa kujijengea mahekalu kana kwamba "wataishi milele".
4). Je watanzania wanafahamu kwamba (Olympic Solidarity inadai kwamba ndio wamelipia gharama za safari ya timu kwenda London!!, pia eti serikali pia ndo waliolipia safari za kwenda London!!). Je watu wenye akili timamu hawapati picha na harufu ya ufisadi?. Je hiyo siyo maana kwamba "hata waziri anapata kigugumizi kuwawajibisha TOC sababu huenda wametafuna wote"?.
MAELEZO MAFUPI KUHUSU NAMBA 4: Inaaminika kwamba (unless they proof otherwise) kuna maofisa kadhaa wizarani pale wenye uwezo wa kuidhinisha fedha, hivyo wanaidhinisha kwamba timu haijalipiwa safari!!, (2004 hadi 2010) wakisha droo hizo hela wanagawana wao na TOC maana safari ilishalipiwa na OS. Pia kuna travel agent moja maarufu jijini Dar (jina nahifadhi) ndo inayotoa risiti feki ili ku - compromise serikalini!!.
5). Je watanzania hawahitaji kujua sababu za mama Pinda kupokonywa zawadi ya Olympic Movement na badala yake kupewa mama Bayi, tena aliyempendekeza ni mumewe, je hiyo siyo matumizi mabaya ya madaraka?.
Ukizingatia hata timu ya Olimpiki kukaa kwa Bayi ilikuwa ni Voting Power ya Bayi maana yeye ni (1) Katibu Mkuu TOC, (2). Mjumbe wa RT, (3) Mmiliki wa Hostel zilizotumika kuandaa timu ya London Games!!.
Kama serikali yetu inahubiri "utawala bora na wa kisheria" inasubiri nini kuunda tume huru kuchunguza madai hayo ili tujue Black or White!!.
MAELEZO MAFUPI KUHUSU NAMBA 5: Olympic Movement ilitaka zawadi apewe mwanamke aliyehamasisha na kuchangia michezo nchini, na jukumu hilo walipewa TOC, inashangaza sana kwamba mama Pinda aliombwa na CHANETA kuchanga fedha ili kufanikisha mashindano ya Africa, tena mama wa watu alijituma na kuonyesha unyenyekevu kwa makampuni makubwa na alifanikiwa kuchangisha mamilioni ya fedha (ambazo matumizi yake hayajawekwa wazi hadi sasa). Lakini katika kilele cha mafanikio
aliyoyasababisha mama yetu mpendwa (TUNU PINDA) zawadi ilikwenda kwa mke wa mtu ambaye (His discretion) ndo ilimuidhinisha mkewe kupata zawadi hiyo kinyemela!!.
Kumbukeni kwamba Meja Bayi anao uhusiano wa
kimasilahi na CHANETA, pia ana masilahi na MPOKEAJI WA ZAWADI yaani mke wake; Je ni nani basi aliye - play a major roll katika kuamua nani apewe zawadi hiyo kama siyo kamanda mwenyewe!!. "Mimi naamini 100/100 kwamba mke wa waziri mkuu ametumika visivyo na hapo TOC wamedhihirisha
kutokuwa na utu!!. Ndo maana hawastahili hata kupewa haki ya kugombea tena, ndo maana tume huru ya uchunguzi itaweza kupembua UKWELI NA UWONGO.
6). Sasa imefahamika "Mystery behind Puma and Lining". Kumbe PUMA ilikuwa inatolewa bure na wadhamini lakini walewale WAIDHINISHAJI wa fedha wizarani (majina tunayo na muda si mrefu tutawataja moja baada ya mwingine), wakawa wana - Bill serikali "kana kwamba Puma hizi hazijalipiwa bado!!, hivyo hela zikitoka zinapigwa mifukoni!!. NDO MAANA SIKU MOJA NIKIWA KTK KIPIMA JOTO LA ITV MHESHIMIWA THADEO ALI BEHAVE KAMA NYOKA ALIYENYANGANYWA PANYA MDOMONI!!, kwani uongo?, watanzania si walishuhudia?. Sasa kama waziri anawaonea haya mafisadi hao mimi nitakwenda hadi Dodoma kuwaomba wabunge wapiganaji kusimamia swala la TUME HURU KUUNDWA DHIDI YA TOC!!, pia tukifikia hatua hiyo majina ya MAFISADI WA WIZARA HUSIKA nitazitaja mbele ya wana jangwani, Msimbazi na wadau wote wa michezo nchini bila kuogopa kuku wala jogoo.
7). Pia wizara na TOC wanatakiwa kuueleza umma iweje wanamichezo waliotuwakilisha London wapate pea moja moja tu ya viatu?. Wakati inaeleweka walistahili kupata begi kubwa lenye vifaa vyote vya michezo sambamba na "memorabilia" zilizowekwa chapa ya 2012 LONDON OLYMPIC GAMES kila mmoja wao. Inaaminika kwamba "kigogo mmoja wa wizara alikwenda London kuwapora wanamichezo mabegi hayo kwa hisani ya TOC ili vifaa hivyo vitumike katika kuwahonga wapiga kura ili BAYI na GULAM warudi madarakani sambamba na timu nzima ya sasa ya TOC ili "mchwa waendelee kutafuta for another 4 yrs".
Do, Ufisadi ulopo TOC ni zaidi ya TANESCO, hapo waziri naye yumo kwani vinginevyo angeshaunda tume!!. Gbuday namkubali kwa kuibua mambo ambayo anayaeelezea kwa ufasaha sana. Bayi kama ana ubavu kwann asimburuze huyo kamanda kortini?. Hana ubavu mana kamanda Buday anamsubiria aende ili ambane kimojaaaa.
ReplyDeleteBayi bado anangangania tu badala ya kujibu mapigo?. Ama kweli ukikamatika ndo hivi.
ReplyDelete