KWA takribani karne nyingi zilizopita inaelezwa kuwa watu walitumia magari yaliyovutwa na wanyama kwa mfano farasi, punda au maksai. Waroma wa kale walifanya majaribio na magari yaliyosukumwa na watumwa. Maendeleo ya uhandisi yalisababisha majaribio ya kutengeneza magari yaliyosogezwa kwa nguvu ya upepo yakitumia tanga kuanzia mwaka 1600 huko nchini Uholanzi.
Hii ilipelekea hata kwenye michezo ambapo mashindano ya mbio za magari yalikuwa yamepitia kwenye historia yake. ASILI YA MBIO ZA MAGARI Historia ya mbio za magari inaeleza kuwa mwishoni mwa miaka ya 1800 michezo ya magari ilianza huko nchini Ufaransa.Hii ilipekea hata mashindano ya kwanza kabisa ya mbio za magari kuanzia huko.
Mashindano hayo yalisaidia pia kubuni aina mpya za magari ya kisasa kadiri miaka ilivyozidi kusonga mbele.
KWANINI MASHINDANO YAFANYIKE KWENYE VUMBI?
Mara nyingi tumekuwa tukishuhudia mbio za magari zikifanyika kwenye barabara za vumbi kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na barabara za lami.
Ukweli ni kwamba sababu kubwa ya mbio za magari kufanyika zaidi kwenye barabara za vumbi inatokana na kwamba kwenye barabara za vumbi gari hukimbia zaidi ikilinganishwa na barabara za lami.
Hii inatokana na sababu za kifizikia ambapo inaelezwa kuwa barabara ya lami ina nguvu ndogo zaidi ya msuguano(Frictional Force) ikilinganishwa na barabara ya vumbi ambayo yenyewe msuguano kati ya tairi la gari na barabara huwa mdogo zaidi.
Sababu za kifizikia pia zinaeleza kuwa bila nguvu ya msuguano hakuna mwendo ambapo hata binadamu hutembea kwa msaada wa nguvu ya mvutano ndiyo maana hata viatu anavyovaa mwisho wa siku huisha soli yake.
Maana yake ni kwamba hata kwenye gari mara nyingi tunashuhudia gurudumu zake zikichoka kwa kuisha na kubaki bila kashata kitu ambacho humlazimu mwenye gari kubadili tairi na kuweka mpya.
Sababu kubwa ni kwamba gurudumu za gari huchakaa kutokana na nguvu ya msuguano kati yake na ardhi ya barabara kitu ambacho ni muhimu sana katika kufanya gari lipate mwendo wa kutoka eneo moja kwenda lingine.
Na Arone Mpanduka(Radio Tumaini) kwa msaada wa mtandao wa Intaneti.mpanduka@yahoo.com
0713896320
No comments:
Post a Comment