Search This Blog

Tuesday, September 25, 2012

JOHN TERRY HANA WA KUMLAUMU ZAIDI YA MANENO YAKE - ATAUJUTIA UAMUZI WAKE

John Terry amestaafu kuichezea timu ya taifa ya England kwa kusema kwamba nafasi yake kwenye timu ya taifa imekuwa njia panda - jambo ambalo sikubaliani nae.

Kama alivyoonesha kwenye Euro 2012 na kwenye mechi dhidi ya Maldova mapema mwezi huu, anabakia kuwa mmoja wa mabeki bora kabisa kuwahi kuvaa jezi ya England.

Ni huzuni kuona amestaafu kucheza soka la kimataifa.
Huu ni uamuzi wa kukurupuka na ameamua kufanya hivi kwa sababu zisizo sahihi.

Hata kama Terry, 31, atafungiwa na FA kufuatiwa tukio lake lilotokea kati yake na Anton Ferdinand, ilibidi vitu hivi viwili na kuendelea kuitumikia England.

Huko nyuma aliendelea kucheza japokuwa kulikuwa na matukio mengi na sijui sasa kwani hajaamua kufanya kama mwanzo.

Hawezi kumlaumu mtu yoyote - matatizo yote yalitokana na maneno aliyoyatoa kutoka kwenye kinywa chake.

Na ninaamini kabisa siku moja Terry atajutia uamuzi wake huu wa kustaafu.

Mwaka 2014, Terry atakuwa nyumbani akiangalia England wakicheza kwenye dimba mojawapo nchini Brazil na Terry atajiuliza mwenyewe "Kwanini nilifanya vile na nikastaafu?"

Ndani ya miaka minne, Euro itachezwa nchini Ufaransa na Terry atakuwa na miaka 35.

Akiwa bila majeruhi katika kipindi hiki chote - angeweza kama kocha angeona inafaa kuwa mmoja ya wachezaji wa kikosi cha England.

Terry anajua atakuwa anamisiwa sana kwenye kikosi cha sasa cha England na ni kweli amekuwa mchezaji muhimu sana kwa Three Lions.

Hata katika mchezo wake wa mwisho, dhidi ya Maldova, alionyesha jitihada zake na kujituma pasipokuchoka huku akikataa kutoka uwanjani dakika 20 zikiwa zimebaki, pamoja na kuwa ameumia.

Kocha wa England Roy Hodgson alikuwa ameshawatumia wabadala wote watatu lakini Terry alijitahidi kutokutoka uwanjani na kuiacha timu yake ikiwa na wachezaji 10, hata kama England ilikuwa ikicheza vizuri sidhani kama Gary Cahili au Jagielka wangekuwa na moyo ule alionyesha Terry.

Na katika mechi dhidi ya Ukraine pale Wembley tukiwa bila Terry uliona tulivyokuwa wepesi nyuma.

Ukweli mwingine mchungu kuhusu suala hili ni kwamba limesababisha mabeki wawili bora wa England kutokuwepo kwenye timu ya taifa kwa sababu nina uhakika Rio Ferdinand nae simuoni akirudi kuvaa jezi za England.

Wote wawili Rio na Terry ni wachezaji wa daraja la dunia. Pembeni ya hao, sioni wachezaji wengine wa daraja lao kwenye timu ya taifa ya England.

Mara ya mwisho nimeonana na Terry ilikuwa kwenye ilikuwa mechi ya golf iliyofanyika eneo la The Groove Hotel pale Hertfordshire wakati wa kiangazi, siku chache kabla ya kwenda Poland.

Niliongea na wachezaji wengi akiwemo Ashley Cole, lakini sikupata nafasi ya kuzungumza na JT ambaye alipotea ghafla. Ni vizuri kama ningepata nafasi ya kuongea nae machache juu ya mambo yalivyokuwa yanaendelea na hatua za kuchukua.

Terry ni mchezaji ambaye ana kariba ya kugawa mawazo, tofauti na wachezaji wengi niliowahi kuwafahamua.

Baadhi ya watu hawampendi na hata kama angestaafu kabla ya tukio lake na Ferdinand, mashabiki wengi wangefurahia kwa sababu tayari alishakuwa sio mtu wao. Wengi wa mashabiki wanaichukia Chelsea hivyo suala lake sio binafsi. Kuna walisnifuata na kuniambia: "Hatuna tatizo na wewe, lakini hatuipendi klabu uliyoichezea."

Pindi atakpostaafu soka kiujumla - nafikiri mashabiki wengi wataangalia nyuma na kuona namna Terry alivyocheza soka na labda watamuheshimu zaidi kuliko ilivyo sasa.

Washindi pekee na wa kweli juu ya uamuzi huu wa Terry watakuwa ni Chelsea na nina uhakika Roberto Di Matteo amefurahia sana.

Kustaafu soka la kimataifa kutamfanya Terry awe na mapumziko zaidi na kuwa vizur kimwili na nategemea kumuona akicheza soka la kiwango cha juu kwa mwaka au miaka miwili zaidi kuliko kama angeendelea kuichezea England.

Atakumbukwa kama mlinzi bora wa Chelsea na England.

Ingawa pamoja na mafanikio yote aliyonayo, lakini siku moja Terry atakapokuwa mkubwa zaidi ataangalia nyuma na atatamani kama angefanya vitu tofauti. Hili linatokea kwa wote.

Kwa kifupi ataujutia uamuzi wake wa kustaafu kwa wakati usio sahihi kuichezea timu yake ya Taifa.

By Ian Wright

No comments:

Post a Comment