Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa ya ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekana kupotoshwa
1. Azam FC ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa siku ya Jumatano 1/08/2012 saa saba mchana na ilivitaka vilabu vyenye interest na mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo zilizopo kwenye kiwanda cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu. Bei ya mauzo iliyopangwa ilikuwa ni Dola 50,000. Lakini katika mawasiliano ya email kwa makatibu wakuu wa Simba na Yanga, Azam FC iliweka bayana kuwa ilikuwa tayari kushusha bei ya mauzo na ingemuuza Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa kubwa zaidi ya mwenzake.
Kwa maana hiyo biashara ya mchezaji mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi. Lengo la Azam FC lilikuwa ni kutoa haki kwa kila klabu yenye uwezo wa kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa.
Pia tunaomba ifahamike bayana kuwa mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na aliombwa asaidie kushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake. Ngasa alitamka bayana kuwa yupo tayari kwenda klabu yoyote ambayo Azam FC itaona imekidhi mahitaji yake kwa masharti kuwa maslahi yake ya kimkataba kati yake na Azam FC yazingatiwe.
2. Hadi kufikia siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba pekee iliyojibu kwa maandishi na kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga wao hawakuwahi kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbe wao wa Kamati ya usajili Bw Sefu Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya zaidi ya milioni 20. Na Yanga haikuwa tayari kuboresha ofa yake.
3. Muda wa kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee kupitia kwa makamu Mwenyekiti wake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake ndiyo waliofika wakiwa na pesa taslimu shilingi milioni 25. Yanga hawakuonekana na hawakutaka kupokea hata simu walizokuwa wakipigiwa kuulizwa kama wana interest.
4. Kikao cha dharura cha Azam FC kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa ilishindikana kutokana na kutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000. Kwa maana hiyo Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo kwenye klabu iliyofika na kuonesha nia ya kumhitaji (Simba)
5. Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba
6. Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki.
7. Azam FC inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa. Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC
8. Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu.
9. Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipo tayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
10. Kwa kuwa Sakata hili limeanza kuhusishwa na sakata la Mchezaji ramadhani Chombo. Naomba nitoe ufafanuzi kama ifuatavyo. Redondo alipewa option tatu za kuchagua baada ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu timu ilipokuwa safarini Mwanza.
a. Kupelekwa kwa mkopo Moro United?
b. Kupatikana kwa mnunuzi mwenye shilingi milioni 40
c. Kukubali adhabu ya kufungiwa kwa miezi mitatu na kulipwa nusu mshahara wahati akitumikia adhabu.
Redondo alithibitisha kuipenda Azam FC kwa kukataa kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo. Alikubali kutumikia adhabu yake na ilipoisha alirudi na kuomba msamaha na sasa ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu sana. Azam FC inajivunia kuwa na mchezaji kama Redondo na bila kupepesa macho wala kung’ata maneno. Azam FC inamchukulia Redondo kama mtu spesho na mwenye mapenzi ya dhati na klabu yake na inamtaka aendelee kuwa na moyo huo.
Imetolewa na utawala.
Azam FC
Hiki ni kichekesho tosha kabisa...sijawahi ona au kusikia kitu kama hiki zaidi ya TZ. Kwa mwendo huu mpira wetu hautaendelea kamwe. Azam wanafuata ule ule mkondo wa vibabu 2( Mnyama na Ndalla)..Nadhani soka letu bado halijapata watu wa kuliongoza wote ni wababaishaji tu...
ReplyDeletesafi sana azamu ci mamieni nidhamu mciwe kama cimba na yanga yakulea wachezaji
ReplyDeleteMdogo wangu ngasa karibu simba ucheze soka, huku kocha anakukubali na ndie aliyekupendekeza. Njoo ufanye kazi achana na maneno ya mtaani.
ReplyDeletetatizo lililopo ni kuwa Ngazsa anamapenzi na Yanga,na Azamu wampeleka simba ili mapenzi aliyonayo kwa Yanga hasiwaabukize wachezaji wengi wa Azamu, la pili nikuwa Ngasa hatacheza mechi ya Azamu na Simba,na mechi ya Simba na Yanga Ngasa hatacheza kwa sababu Simba wanajua wakifungwa lawama zote zitakuwa kwa Ngaza sasa kati ya Simba na Azamu nani kapatikana mwanasport?
ReplyDeleteNaungana na mtoa maoni wa kwanza hapo juu.
ReplyDeleteKilichofanyika katika sakata hili ni usanii mtupu na wala hakisaidii jitihada zetu za kukuza soka nchini.Ni usanii kama usanii wowote wa kitapeli na mwenye kuumia ni: Ngasa na Soka la TZ na wapenzi wake.
Ngasa atacheza SSC kwa maluweluwe hilo halipingiki. Tuliyaona hayo kwa Zamoyoni Mogella na JUma Kaseja.
Upenzi (faantism)wa Yanga na Simba unapita hata ule wa dini hapa nchini. Ni rahisi kwa m-TZ kujitangaza imani yake ya dini kuliko kujitambulisha kuwa ni mpenzi wa Yanga au Simba. Sasa ikishaeleweka kuwa wewe ni Yanga au Simba; huwa ni vigumu sana (kama vile haiwezekani) kuwaaminisha watu kuwa sasa wewe umebadili mapenzi yako toka Yanga kwenda Simba (na kinyume chake). Ilitokea hivyo kwa Bw. Abdallah Majura (yule mwana-habari maarufu nchini) alipotangaza kuwa amehamishia ushabiki wake Simba toka Yanga. Nobody trusts him 100%.
Kituko cha pili ni kwa Ngasa mwenyewe. Kijana huyu amethibitisha namna wa-TZ tusivyo na ustaarabu wa kusema kile kilicho ndani ya mioyo yetu. We don't digest what we intend to speak out. Hatutafakari.
A day before yesterday Mrisho alisikika akiwananga viongozi wa SSC na Azam kwa kutangaza kuuziana mchezaji huyo bila kumshirikisha. Alisema hakuwa tayari kuuzwa kama fungu la nyanya mbovu. Nadhani alichopaswa kuema (kwa kuwa hakuwa amepata taarifa kwa kina ni " naomba nipe muda nitafakari habari hizi kabla ya kukujibu swali lolote maana sijawasiliana na viongozi wa Azam wala wale wa SSC".
Hii ingempa fursa ya kutafakari na kupanga vema mawazo yake na kutoa majibu yenye mantiki.
Vijana wetu kama Mrisho wanapaswa kujielimisha jinsi ya ku-deal na waandishi wa habari.
Swalle gfs