Nuri Sahin - Mchezaji wa Real Madrid na Uturuki |
Bilali Ahmed maarufu kama Frank Ribery akiwa na mchezaji Hamit Altintop walipoenda Makka |
Samir Nasri na utukutu wake wote mwezi huu yupo ndani ya mfungo |
Karim Benzema |
Hatem Ben Arfa - Kiungo wa Newcastle na Ufaransa nae nafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani |
Mesut Ozil - Raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki |
Samir Khedira - Raia wa Ujerumani mwenye asili ya Tunisia. |
Abdulsalaam Bilal maarufu kama Nicolas Anelka akiwa na mashekhe alipoenda hijja huko Makka |
Bilal Abidal - maarufu kama Eric Abidal akisoma Quran akiwa kwenye ndege wakati akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa mwaka jana. |
Anaitwa Ibrahim Affelay mchezaji wa kimataifa wa Barcelona na Uholanzi |
HII NI VIDEO INAYOMUONYESHA THIERRY HENRY AKITHIBITISHA KUBADILI DINI NA KUWA MUISLAM AKIFUATA MFANO WA RAFIKI ZAKE ANELKA, NA ABIDAL.
Mashallahh
ReplyDeletehi! blogger kiukweli sijakuelewa nia ya wewe kupublish hii habari.kimtazamo wangu naona kama unaudini ndani, nahii kitu inaanza kuota mizizi katika jamii yetu.ukiwa kama chombo cha habari jitahidi sana kutokujenga makundi kwa wale unao wapasha habari
ReplyDeletePost yako haina maana yoyote katika michezo..udini umekukaa tuu badala ya kuangalia maisha yako yalivyo duni na jinsi gani ya kupata mafanikio ya kimaisha unafikiria upuuzi huu...Stupid journalist
ReplyDeleteSioni udini hapo kwan tatizo likowap
ReplyDeleteNyie ndiyo wadini yaani Rooney alivyosema atakuwa pastor ilikuwa sawa hawa wameoneshwa wanafunga mnadai udini! Mjiamini na imani zenu kila mtu anachagua anapoona sawa hivyo wana michezo wana dini zao sasa wakioneshwa wana abudu dini zao mnadai udini....acheni hizo
ReplyDeletekatika post za kijinga ulishowahi kupost ni hiii, what is the essence of the post? ulikuwa unamaanisha nini au ulitaka kufikisha ujumbe upi? mbona unazunguka zunguka sanaaaaa kuwa straight kaka or whatever u call ru self? kufunga ama kutokufunga ni mtu mwenyewe hata kuwa muislamu au mkristo ni swala la mtu binafsi acha utoto weka post zenye maana. ukitoka kuwaandika hawa andika na wanaofunga kwaresma kama utaweza pia uje na kwa wale wasioamini kama kuna Mungu usiishie hapo. Acha upopolimpoo
ReplyDeleteShafii unge post hao jamaa wamekuwa freemaons, ungeona comments za kukupongeza kibao, lkn kwa kuwa muslim imeshakuwa tatizo, cha kushangaza hadi wengine wanatoa matusi, sasa sijui kuandika habari inyohusu uislam ndio ujinga au! Kuweni fair jamani, jamaa wamesoma wakaelewa na kufuata haki, nyinyi tukaneni tu bila ya kutafuta ukweli, mtakuja kumbuka shuka kumekucha.
ReplyDeleteWe shaffi acha utoto wewe..kwani kuna mtu alimzuia Mike Tyson kuwa mwislamu? au unafikiri hatujui hilo,kwa nini hujiamini? haya sasa hao watakusaidia nini
ReplyDeletewanakupa chakula? wamekujengea nyumba? wamekununulia gari? wanakusomeshea watoto wako? Unapata nini toka kwa hao?..nafikiri kichwa yako imejaa utoto
huyo Shafii ndo hajiamini na anataka kutuonyesha kuwa hao wachezaji ni waislamu kitu ambacho ni stupid, mtu kuwa Muislam au la Ni maamuzi binafsi hakuna waliowalazimisha ni wao wenyewe. Jiaminini na IMANI zenu sio lazima kuwaonyesha watu and then what for?? usisahau kuandika wasioamini pia (Atheist) JIAMININI SIO LAZIMA KUTANGAZIA WATU
ReplyDeleteKama waislamu wenye mafanikio mbona wengi tu! Kwani hatujui kuwa wamiliki wa Man City ni waislamu? wapo wafanyabiashara wengi tuu wa kiislamu wenye kumiliki visima vya mafuta huko Saudi Arabia na wengine wanamiliki timu...kwani kuna mtu alimuuliza Shaffi kuwa hakuna wachezaji nyota wa Kiislamu?.
ReplyDeleteWengine hushabikia wachezaji bila kujali rangi,dini au kabila lake..Sisi huwapenda kwa kuwa ni wachezaji bora na hatuwapendei dini yao au rangi yao...Wote tunajua kuwa kuna Madoctors,Engineers,Scientists,Politicians,Football players,Boxers,Athletics n.k ambao ni waislamu...JIAMINI
Wanaopinga wote hao ujue ndo wale kinananihino ambao wanuumwa kuona habari hizo . Hii blog ya michezo na hao ni wana michezo. Na kwa uislam dini mfumo mzima wa maisha hauwezi kutofaitishwa na maisha .sasa kama nyie kina nanihino mna dini mbali na maisha mengine mbali ilo lenu msitake kutbalisha na sie kila mtu na upeo wake . Big up bin Dauda.
ReplyDeleteHii migalalatia mm inaniuzi kweli.Aa nn tatizo hapo na Hii ni mwezi mtukufu.Basi ukipost wachezaj wanavyosherehekea x mas watasifu..stupid
ReplyDeleteJamani ninini lakini? kwani hii blog c inahusiana na michezo na maisha ya kila siku ya wanamichezo? Mbona mnakosa uungwana kiasi hiki? wanavyoandikwa freemason ndio mnakua na kimbelembele, 2badilike jamani hizi ni habari za wanamichezo na zimeandikwa wakati wa mfungo wa ramadhani. kwani ikija kwaresma si ataandika pia kama nyuzi hizo zikiwepo. msilete udini kiasi hiki yaani inaonyesha wazi wazi ni jamiii ya wa2 fulani ndio wanaopinga hizi habari. Hebu kuweni Fair na muangalie kama hata andika katika mfungo wa kwaresma kama pia nyuzi husika zitzkuwepo.
ReplyDeletekeep it up brother,wewe pia ni binadamu ya unaimani yako,kwani ukiwa muandishi wa habari hupaswi kugusia hata kidogo dini?roho zanawauma kuona mtu kama anelka kuwa alhaji !!!!nashukuru kwa kutuhabarisha
ReplyDelete