Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba, leo mchana walikutana na mchezaji mwenyewe ili kuweza kukubalina juu ya mahitaji yake binafsi, baada ya jana wekundu hao wa msimbazi kumalizana na Azam.
Kwenye mkataba wake mpya na Simba, Ngassa atapewa gari aina ya Verossa, ada ya usajili millioni 30 pamoja na kupewa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi kama alivyokuwa akilipwa kwenye klabu aliyotoka ya Azam.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari mkataba ni mwaka mmoja.
simba wanatapatapa baada ya kuvurunda kagame.tusubiri tuone kama ngassa ataweza kuwavusha kwenye mawimbi yanayowakabili hivi sasa.thamani ya ngassa na mchango wake uwanjani itabidi viende sambamba,vinginevyo muda mfupi tu ataanza kuzushiwa kwamba anahujumu timu kwani tunawafahamu mashabiki wa simba na viongozi wao walivyo vigeugeu.hayo yaliwakuta akina,Banka,Mukenya,Barasa,Lunyamila,Mmmachinga,Malima,Omari Hussein,Athumani China,Mtwa kiwelo,Tigana,Mulumba,Silvatus Ibrahim,Rajabu Mwinyi ambao walisajiliwa kwa mbwembwe na baadaye kutoswa kwa aibu
ReplyDeleteNini maana ya kutapatapa?kusajiri mchezaji haimaanishi kuwa timu inatapatapa simba wamegundua udhaifu kwenye kikosi ndio maana wanajipanga upya acheni kelele kama 'Inzi'Yanga haina pesa mwenye pesa Manji sasa mwenyewe kagoma kwakuwa dau lake dogo m20 sasa simba wameingia kwa dau kubwa sasa hivi tusubiri tuone simba wamelamba dume ama garasa?.
DeleteHatumtaki Simba huyo! Ina maana mechi zote tukicheza na Yanga hatacheza huyo maana yeye ni Yanga damu!
ReplyDeleteKamanda wa ukweli,kambi popote,kila la heri uendako"simba" ,lakini wakikuzingua tu,you must back home.
ReplyDeletehahahah mbona hawajasema ni mkataba wa muda gani
ReplyDeleteHaya ni Maisha tuu,Mwachen Ngassa aende popote ilimradi Maslahi yawe Mazuri...!
ReplyDeletekama kweliNgassa ana nia na mpira na mpira ni kazi yake basi aheshimu maamuzi aliyoyafanya kuchezea simba aachane na upenzi wakizamani tutaendelea kuwa wapinzani ila inapofikia swala la maendeleo basi afanye kweli aaachane na ushabiki namtakia maisha mema na yafuraha msimbazi acheze vizur simba haina tatizo na m2 baaaaaaaaaaaaaaaaaaac
ReplyDeleteNgasa aina ya uchezaji wake utamcost,labda acheze kama forward no 10 pale simba ajifue kweli kweli.karibu simba ngasa!!!!
ReplyDeleteNgasa aina ya uchezaji wake utamcost,labda acheze kama forward no 10 pale simba ajifue kweli kweli.karibu simba ngasa!!!!
ReplyDeleteCha mgema huliwa na mlevi..!
ReplyDeleteNgasa awache ushabiki wake wa Yanga. Proffessional footballers huweka ushabiki pembeni na kutumikia kwa moyo wote club zao. Nadhani amepata funzo baada ya Azam kumtupia virago.
ReplyDeletewana yanga mnafurahisha sana, eti watamgeuzia kibao! hilo mnaliona kwa simba tu? mlishatimua timu nzima akabaki kimanda tu baada ya kupigwa nne kwa moja na mnyama, au mmesahau? na baada zile tano za juzi mtuhumiwa namba moja alikua nurdin bakari.ama hakika nyani haoni kundule! ngasa acheze mpira na aache unazi kwani ndio uliomuondoa azam. wapo watu kama kina beckham alishasema yeye ni mchezaji wa madrid lakini mshabiki wa man u. walcot mchezaji wa arsenal mshabiki wa liverpool, kwa hiyo kupenda timu nyengine na kucheza timu nyengine sio hatari ila kinachotakiwa ni uwajibikaji.
ReplyDeletekwa upande wangu sioni kama atakuwa msaada msimbazi hicho kitakuwa kirusi tu kwenye mechi angeenda zke jangwani huyo hata kama mpira kwake ni kazi bado mapenzi yake ni yanga ko mezi za simba na yanga atakuwa hachezi sababu anajua msimu ujao atakuwa yanga tu.
ReplyDeleteHaina shida hata kama Ngasa ni mnazi wa Yanga. Mbona Kaseja ni mnazi wa Simba lakini alienda Yanga na alicheza bila shida then akarudi zake Simba. Hawa wachezaji ni professionals bwana na mpira ndo maisha na kazi yao.
ReplyDeletekwa jinsi swala la Ngassa lilivyoanza hadi kumalizika kwa Ngassa kukubali kucheza simba,2013-2014 Ngassa atacheza yanga.
ReplyDeletenadhani simba watakua wameshatambua nini maana ya maneno "MJINI SHULE" mnamchukua mchezaji kwa mkopo, mnawapa azam pesa mingi, mnamlipa mchezaji mshahara mkubwa, mnampa booonge la mkoko alafu mwisho wa siku haki zote za kummiliki mchezaji bado ziko azam..............dah poleni sana bandugu ila hata hivyo kawasaidia kushika nafasi ya tatu kwenye ligi, nafasi ambayo hamkustahili kushika kwa mwaka huu.
ReplyDelete