Eleweni kwamba kuna vijana ambao walikuwa tayari kwenda Melbourne kuiletea Tanzania medali, hata VISA walishapata kwa kufikia vigezo vyote vya kushiriki mashindano ya COMMONWEALTH GAMES, kambini wamekaa na kujiandaa vyema na walikuwa na furaha sana kwenda kuwa mabalozi wazuri. Hata suti walishapimiwa na baadaye walinyanganywa dakika za mwisho kibabe!!.
Walinyimwa kwenda kwa sababu zifuatazo:
1). Rogati ni kijana wa JOHN STEPHEN AKHWARI (yule mzee wetu
aliyetuwakilisha Mexico Olympics 1968), Australia wanamthamini na
kumheshimu sana mzee huyo, hivyo waliandaa mpango wa kum-enzi mzee wetu
kupitia kijana wake, waliandaa mpango mzuri wa kuhoji na hata kumpa "TV
ADDS, mheshimiwa Bayi hakupendezewa na hilo ndiyo maana akabuni "emergency
plan" ya kumzuia kijana huyo maana "ange take over media attention". bila
kujali medali itakayoletwa Tanzania na Rogati!!.
2). Ili kuweka "kiini macho" MICHAEL MISLAY naye alipigwa nje "ili
watanzania wasijue sababu halisi ya kijana wa JOHN STEPHEN kupigwa nje
ghafla. Hiyo ni medali ya pili inapotezwa kwa ajili ya WIVU WA MTU MOJA!!.
Eti sababu waliyoelezwa ni kwamba "tume - misplace passports zenu na hatuna
muda wa kuzitafuta!!.
3). Nafasi hizo mbili hazikuachwa wazi maana walipewa watu ambao walikwenda kufanya biashara zao ambazo bila shaka WATAGAWANA NA BOSI HUYO WA TOC!!. JE, TUSIPOYASEMA MAMBO HAYA SISI VIJANA AMBAAO NDIYO TAIFA LA KESHO; NANI ATAYASEMA?. VITHIBITISHO HIVYO HAPO JUU (Attachments) KUWA HATA VISA WALISHAPATA. (Mimi nasisitiza uchunguzi ufanywe na serekali kupitia BMT na ikithibitika hatua zichukuliwe kwa waliohusika bila kujali vyeo vyao. (Tunaongelea masilahi ya Taifa siyo ya Bayi).
Mbona kama kuna zaidi ya hayo?umejuaje kama hawa jamaa wangeleta medali?kila jambo na wakati wake,inawezekana wakati wake wa kufichua ni sasa,why haukusema hizi sababu walipotudanganya au kwa sababu umekosa uongozi hivyo una chuki?
ReplyDeletekama kweli bayi kafanya kusudi na alaaniwe maisha
ReplyDeleteUnajua nashindwa kukuelewa, ulikuwa wapi miaka hiyo yote 6 iliyopita mpaka uje kusema leo?? sikatai waweza kuwa unasema ukweli ila napata sana wasiwasi na wewe..kiukweli hii imekuja baada ya kushindwa uchaguzi..acha chuki binafsi ww, ungekuwa muwazi na msafi ungesema tangu kipindi hicho..nawe ulikuwa miongoni mwao au ulipewa chochote. Sa umekosa ndo unajidai kusema ukweli.Be a gentleman at right time..ila ahsante kwa taarifa nzuri, umetufumbua macho!
ReplyDelete