Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, aliiambia tovuti ya Simba kwamba usitishwaji huo umefanyika kwa makubaliano ya pande zote mbili (Simba na Machaku) na kwamba kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania sasa ni mchezaji huru.
Machaku alisajiliwa na Simba msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili uliotarajiwa kumalizika mwakani lakini kwa maamuzi haya, sasa anaweza kujiunga na timu yoyote anayopenda.
"Kwa niaba ya klabu ya soka ya Simba, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Machaku kutokana na kazi kubwa aliyoifanya msimu uliopita ambapo timu yetu ilitwaa ubingwa wa Tanzania na kuwa timu bora.
"Machaku alikuwa sehemu muhimu ya timu yetu na ndiyo maana hatuna neno baya la kusema juu yake zaidi ya kumtakia maisha marefu yenye heri na fanaka. Huwezi kujua inawezekana wakati mwingine akarejea tena Msimbazi na kuwa mchezaji muhimu," alisema.
simba watajuta kumuacha alikuwa na msimu mgumu kwa kuwa ilikuwa first time anacheza timu kubwa tz,, tatizo timu zetu zinaongozwa kisiasa sanaa,, kuweni makini jamani
ReplyDelete