Search This Blog

Tuesday, July 17, 2012

CRISTIANO RONALDO AMFUNIKA LIONEL MESSI KWA UTAJIRI - FLOYD MAYWEATHER ASHIKA NAMBA MOJA LISTI YA WANAMICHEZO WANAOLIPWA FEDHA NYINGI 2012



Bondia wa kimataifa wa Marekani aliyepo jela kwa sasa Floyd Mayweather Jr. ametajwa na jarida la Forbes kuwa ndio mwanamichezo anayeingiza fedha nyingi kwa mwaka, akiwa amepeleka banki dola millioni 85,000,000 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Mayweather anafuatiwa na mpinzani wake mfilipino Manny Pacquiao aliyeingiza kiasi cha $62 million.
Wacheza soka matajiri zaidi duniani.
                      
Pamoja na mchezo wa soka kuwa ndio maarufu zaidi lakini wacheza soka wenyewe wameshindwa kuingia hata kwenye Top 5, ingawa wapo kwenye 10 bora. Muingereza David Beckham akishika nafasi ya nane kwa kuingiza millioni 46 USD, huku akifuatiwa na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye amepeleka bank kiasi cha $42 million. Mchezaji bora wa dunia wa soka Lionel Messi hayumo kwenye top 10, japo hayupo mbali akiwa nafasi ya 11 kwa kuingiza kiasi cha $39 million.
Mchezaji anayelipwa zaidi kwenye lgi kuu ya England
Mcheza soka mwingine aliyepo kwenye 50 bora ni Wayne Rooney nafasi ya (37) akiingiza $24 million - akiwa ndio mchzaji pekee wa ligi kuu ya England aliye kwenye Top 50 ya wanamichezo wanaolipwa fedha nyingi duniani.


#1 Floyd Mayweather
Total earnings: $85 million

#2 Manny Pacquiao
Total earnings: $62 million

#3 Tiger Woods
Total earnings: $59.4 million

#4 LeBron James
Total earnings: $53 million

#5 Roger Federer
Total earnings: $52.7 million

#6 Kobe Bryant
Total earnings: $52.3 million

#7 Phil Mickelson
Total earnings: $47.8 million

#8 David Beckham
Total earnings: $46 million

#9 Cristiano Ronaldo
Total earnings: $42.5 million

#10 Peyton Manning
Total earnings: $42.4 million
*******************************************************
#11 Lionel Messi
Total earnings: $39 million

No comments:

Post a Comment