Search This Blog

Wednesday, June 6, 2012

KWANINI MANJI ANAUTAKA UONGOZI WA YANGA?

*NI KWELI ANATAKA KUIMILIKI YANGA?

*NA KAMA AKIFANIKIWA KUWA MMILIKI ATAIFANYIA NINI YANGA?

*KWANINI BAADHI YA WANACHAMA HAWAMTAKI?


Kwa kipindi kirefu sasa tangu mfanyabiashara maarufu Bwana Manji ajiingize katika kuifadhili klabu ya Dar Young Africans kumekuwepo na mgawanyiko mkubwa wa kifikra miongoni mwa wanamichezo, wanachama na wapenzi wa Yanga, juu ya madhumuni hasa kabisa ya mfanyabiashara huyo kuisadia Yanga.

Huku baadhi ya watu wakisema Manji ana nia ya dhati kabisa ya kuisadia Yanga na kuifanya kuwa klabu ya kisasa kabisa,huku wengine wakibaki kusema kwamba mmiliki huyo wa Quality Group of Companies anataka kuitumia Yanga kibiashara na kujinufaisha binafsi kwa kutumia brand ya Yanga.

Katika kipindi cha awamu mbili za uongozi tofauti pale Yanga, kuanzia kwa Wakili Iman Madega mpaka uongozi huu uliopinduliwa wa mwanasheria Lloyd Nchunga, Yusuph Manji amekuwa akitajwa kuhusika na migogoro mikubwa iliyojitokeza ndani ya klabu hiyo.

Hivi karibuni baada ya baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga hasa wakiongozwa na wazee wa klabu hiyo, waliongoza mapinduzi ya kuuondoa uongozi halali wa bwana Lloyd Nchunga, ambaye mara ya kwanza  alijaribu kutuna lakini mwishowe akaachia ngazi mwenyewe baada ya kuandamwa sana kiasi cha kuanza kupokea vitisho na kufanyiwa vurugu. Wazee wakachukua timu huku wakitamba wana zaidi ya millioni 750 za kufanya usajili, lakini TFF ikairudisha timu chini ya uongozi wa katibu mkuu Celestine Mwesiga huku wakiagiza ufanyike uchaguzi kama katiba ya klabu inavyosema.

Uchaguzi ukaitishwa kwa mujibu wa kanuni, na kamati ya uchaguzi ikaanza kutoa fomu za nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Yanga.


Katika hali ya kushtusha siku ya jumatatu mfanyabiashara na mdhamini wa klabu hiyo, Manji akachukua fomu ya kugombea uenyekiti wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya jangwani,huku akimchukulia mmoja wa wajumbe wa kamati ya usajili Abdallah Ahmed Bin Kleb fomu ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji, na hatimaye leo Manji alikuwa mmoja ya wanachama 29 wa Yanga waliorudisha fomu za kugombea nafasi za uongozi mbalimbali ndani ya Yanga.

Kitendo cha Manji kuutaka ubosi wa klabu ya Yanga umeibua hofu na maswali mengi juu ya nia hasa ya mfanyabiashara huyo dhidi ya Yanga, baadhi ya wanachama wa klabu hiyo ambao siku zote wamekuwa wakimpinga Manji kwa namna moja au nyingine wakidai hana nia nzuri ya klabu yao, wameongea exclusively na shaffihdauda.com na kutoa hoja nyingi sana zinazojaribu kuelezea kwanini hawana imani na mpango wa Manji kuwa mwenyekiti wa klabu yao.

1:MANJI VS IMANI MADEGA NA LLOYD NCHUNGA

Wakati wakili Iman Madega anataka kuingia Yanga alikuwa akipigwa tafu kubwa sana na bwana Manji mpaka akafanikiwa kuutwa uongozi wa klabu hiyo. Lakini baada ya muda kupita kukatokea kutokuelewana baina ya watu hao wawili. Hii ilikuwa ni baada ya Manji kuleta wazo la kutaka Yanga iendeshwe na kampuni. Kwa maana ingeanzishwa kampuni ambayo ingenunua asilimia 51 za Yanga, na asilimia 49 zinazobakia zingekuwa zinamilikiwa na wanachama ambao wangekopeshwa kiasi cha billioni 3 na Manji kwa mkopo wa mwaka mmoja tu, huku akiwawekea sharti kwamba kama wangeshinda kuzilipa billioni 3 zake alizowakopesha ndani ya kipindi walichokubaliana kulipwa na mkopo huo , basi Manji ndio angekuwa mtu wa kwanza kuuziwa hisa zile zile ambazo walishindwa kuzilipia.
Pia katika zile hisa asilimia 51, hakukuwa na sheria zozote za kumkataza mtu yoyote kununua hisa hizo, uwe mwanachama au la ungeweza kununua hisa, hata Manji mwenyewe kama angejisikia kufanya hivyo pia alikuwa na uhuru wa kununua.
Baada ya kuupitia vizuri mpango huo Iman Madega hakuweza kukubaliana na mpango huo kwa hofu, kwamba ule ni mpango ambayo ungeidhuru Yanga.

Baada ya kumshindwa Madega ambaye alifanikiwa kumaliza kipindi chake cha Uongozi, klabu hiyo ikafanya uchaguzi na kupata uongozi mpya chini ya Lloyd Nchunga ambaye naye alipoletewa mpango wa kuanzishwa kwa kampuni na Manji akakataa na matokeo yake timu ikahujumiwa kitu kilichopelekea migomo ya wachezaji, na hivyo timu kufanya vibaya kwenye ligi. Inasemekana baada ya Nchunga kuvimba na kukataa kujiuzulu baada ya kipigo cha 5-0 kutoka watani wao Simba, ndipo bosi Manji alipoanza kutoa mkwanja kwa baadhi ya viongozi na kuwaambia wajiuzulu huku akiwatumia wazee kumtia mshikemshike Nchunga ambaye mwishowe akaamua kujiuzulu na kupelekea kuitishwa kwa uchaguzi mpya.


 KIVIPI?

Kiuhalisia tu shilingi billioni 3 ni fedha nyingi sana kwa wanachama wa kawaida wa Yanga ambao ndio wapo wengi kuweza kumudu kuzilipa ndani ya kipindi mwaka mmoja. Hata kama wangemudu kuzilipa basi isingekuwa rahisi unless kuwe kuna mkono wa mtu nyuma yao, na kama wangeumudu kwa uwezo wao basi ni wachache sana wangeweza kufanya hivyo, hivyo mwisho wa siku hisa nyingi sana zingerudi mikononi mwa Manji.
Huku pia kwenye asilimia 51 za kampuni  Manji alikuwa na uhuru wa kununua hisa, hivyo kama Manji akazipata labda asilimia 40 ya hisa alizowalipia wanachama kwa mkopo na wakashindwa kuzilipa na huku kwenye kampuni akanunua japo asilimia 15 tu, kwa maana hiyo angekuwa ndio majority shareholder hivyo kumfanya kuwa mmiliki wa Yanga SC.

2: KWANINI HAWATAKI MANJI AIMILIKI YANGA?
Anti-Manji wanasema hawana imani kabisa na Manji kwamba anaitaka Yanga ili kuisadia iwe klabu na yenye mafanikio, bali ni kwa maslahi yake binafsi.
Kwanza wanajenga hoja kwamba Manji hakuingia Yanga kwa mapenzi binafsi bali  alisukumwa na sababu za kisiasa kwa kuifanya klabu hiyo inayosadikika kuwa na wapenzi wengi zaidi nchini kuwa kichaka cha kujifunikia madhambi yake baada ya kukumbwa na kashfa ya EPA.
Wanasema Manji tofauti na wadhamini wengine waliowahi kuidhamini na kuisadia Yanga kama akina Gulamali na Mohamed Vilani, ambao walikuwa wakitoa fedha nyingi kuisadia timu yao bila kuidai chochote, lakini Yusuf Manji siku zote amekuwa akiwasainisha kwenye vitabu vya kumbukumbu viongozi kwa niaba ya Yanga kila anapotoa fedha labda ya usajili au kuisadia pale timu inapokwama kiuchumi, na hilo limeshathibitishwa na Manji mwenyewe pale alipokaririwa mara kadhaa akisema anaidai Yanga fedha nyingi bila kuweka wazi ni kiasi gani. Kwa hiyo hawajui ni lini atawadai fedha anazoidai klabu hiyo na kama watashindwa kulipa je atafanya nini?

Anti-Manji wanaendelea kujenga hoja zao kwa kusema kuwa wanahisi kwamba Manji ambaye pia ni mfanyabiashara ambaye anamiliki majengo mengi ya kibiashara hapa nchini anachokihitaji kutoka Yanga kwanza ni kujilipa fedha zote alizotumia kuisaidia klabu hiyo pamoja na zile ambazo zipo nje ya vitabu alizotumia kupata wafuasi waliochini ya himaya yake ndani ya klabu hiyo.

Wanasema wasiwasi wao ni kwamba ikiwa Manji atakuwa mmiliki wa Yanga, ataitumia brand ya klabu hiyo pamoja na assets zake ili kujilimbikizia fedha nyingi kwa kipindi labda cha miaka 3 mpaka mitano na baadae ataliuza tu jina la Yanga ikiwemo timu, na yeye kubaki na assets za Yanga yakiwemo majengo mawili ambayo yote yapo kwenye eneo la kibiashara la kariakoo pamoja na eneo kubwa wanalolimiliki Yanga la Jangwani makao makuu ambapo imegundulika Yanga inahodhi eneo kubwa sana ambalo kwa sasa limevamiwa na baadhi ya majirani wanaoishi karibu na makao makuu ya Yanga-Jangwani.

Endapo Manji ataliuza jina la Yanga na kubaki na assets za klabu hiyo kisha kuzitumia kwa matumizi mengine, klabu hiyo itapoteza sehemu ya historia yake kubwa iliyojijengea.


3: ANTI-MANJI WALIVYOPOKEA TAARIFA ZA MANJI KURUDISHA FOMU BILA TEGEMEO LAO IDD KIPINGU KUSHINDWA KUCHUKUA FOMU.

Baada ya Manji kuchukua fomu za kugombea uenyekiti wa Yanga, kundi la wanachama wanaompinga Manji kwa sababu zao waliamua kutafuta njia za kuweza kupambana nae. Inasemekana wakajaribu kumtumia mtoto wa kigogo wa nchi ambaye nae ana nguvu na ufuasi mkubwa ndani ya klabu hiyo,  ili aweze kumshawishi Kanali Iddi Kipingu agombee nafasi hiyo, lakini baada ya Kipingu kushindwa kuhakikishiwa kupewa sapoti ya asilimia 100 ya kuweza kupambana na tajiri Manji akaona bora asijiingize kwenye vita mabayo itaweza kumshushia heshima yake kubwa aliyojijengea kwenye tasnia ya michezo nchini kwa kuangushwa vibaya na Sheikh Mansour wa Tanzania.

NB: HUU SIO MTAZAMO WANGU BALI NI MTAZAMO WA WANACHAMA WA YANGA WANAOMPINGA MANJI. NIMEWASILISHA. BY SHAFFIH DAUDA.

31 comments:

  1. Asante kwa kutujuza suala hili kwa ukaribu kabisa. Mengi tutayajua

    ReplyDelete
  2. Shaffii usipandikize chuki ndani ya Yanga, ni wakati wa wanayanga kujaribu kitu kipya. Kwa mtazamo wangu Manji anamengi ya kuipa Yanga kabla ya kufaidika.

    ReplyDelete
  3. Shaffii usipotoshe wanayanga. Kwa mtazamo wangu ni wakati muafaka kwa Yanga kujaribu kitu kipya. Vilevile Manji ana mengi ya offer Yanga kabla hajafanikiwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hv huyu shafii antumwa na nani?

      Delete
  4. Kaka habari?

    Wewe ni mtu niliyekuwa nakuheshimu sana. Ondoa Usimba wako andika vitu vya kweli. Mtoto wa kigogo, wewe una uhakika gani? nimechoka na majungu yenu. We acha Yanga...tuache na Yanga fanya mambo yako. Kama nilivyosema hapa awali, nilikuwa nakuheshimu sana. Nimechoka na maneno yenu yasiyo na maana, kila mahali ni mtoto wa kigogo, mara hili, mara lile, wewe siungetaja tu jina langu.

    ReplyDelete
  5. utaumia sana ndugu yangu we yanga haikuhusu na wala huusiki nayo, endeleza umbea clouds achana na yanga yetu.

    ReplyDelete
  6. Sasa hapo bwana shaffih unapandikiza chuki live bila chenga

    ReplyDelete
  7. Hakuna lolote, alitaka tujue yupo Ulaya, mara aha naenda Sweden nitaweletea taarifa za wachezaji wa Kitanzania na maisha yao binafsi nje ya uwanja, mara nimefanya interview na Kocha wa timu ya taifa ya ujerumani...wadanganye hao hao, bila clip hapana. Sasa leo from no where, ameandika habari ndefu juu ya Yanga, ukiisoma utaona ameegamia upande mmoja. Article yake hipo upande wa wale wanaompinga Manji ndio ameongelea kwa kirefu na mifano, but ajaangalia mazuri walau aliyofanya Manji. Utakiwa kuwa na Elimu ya kidato cha sita kulitambua hilo. Kaka badili blog yako iwe Simba FC, then tutaelewa moja. You have to be fair, nadhani taaluma yenu inasema hivyo, pia inasema ufanya research kabla ya kuandika vitu vya uongo or hearsay.

    ReplyDelete
  8. hivi hao wanaompinga Manji wameifanyia nin Yanga mpaka muda huu,club imeendelea kuwa masikin,Manji ameisaidia Yanga tangu mgogoro uliomshinda Mengi,mshahara kwa wachezaji na ukarabati wa majengo,atasema uyu m2 ana nia mbaya na Yanga? na club ikiwa na ukata na migogoro ndo hao wakwanza kuomba msaada kwa Manji.Ikitokea Manji anataka kufanya jambo zuri hisia hasi zinaanza kusambazwa kama izi,Mpeni Manji 2one ataifanyia nin Yanga na soka la Tanzania, 2ache unafiki,kaka Shaffih acha ku2mika kwa manufaa ya soka la Tanzania. cku zote 2kumbuke 'WASIO SOMA NI CHAKULA CHA WASOMI'

    ReplyDelete
  9. Mtazamo wa wanaompinga Manji wapi, ni mtazamo wako na usimba wako, acha ushamba kaka. Mapenzi hayo mabaya ndiyo maana wabongo tunakufa maskini. Manji amefanya mambo mangapi? kama ni msimamo wa wanaompinga Manji, mbona hujaandika msimamo wa wale wanao mkubali? acha wewe, hili haliitaji Elimu ya kidato cha sita kulielewa, wewe endelea kutumiwa na Simba wako hao.

    Mdau
    Maryland

    ReplyDelete
  10. Shaffih hii ni habari ya uchochezi hata kama sio maoni yako jaribu kuangalia habari za kupost hata kama wanaokutuma wanakupa hela nyingi

    ReplyDelete
  11. SHAFFIH DAUDA UNAJISHUSHIA SANA HESHMA YAKO, HATA MTOTO MDOGO ANAJUA KUA HABARI HII IPO KINAFKI NA HAIJABALANCE..... WAACHIE YANGA YAO SHAFFI, MBONA UNASHUPALIA HIVYO..... HAKUNA ASIYEKUJUA WW UKO TIMU GANI HAPA TZ, USIFANYE KAZI YAKO KISHABIKI KAKA, MICHEZO NA UDAKU HAVIENDANI!

    ReplyDelete
  12. bro Shaffih kweli heshima yangu kwako imeshuka tena sn, Why are you attacking Manji like that'? Umetumwa na Mengi nn? Make media zake ndo hazitangazi kabisa kama amechukua form? Acha hizo bro, waweza kuwa mkwel ila kwa hili umeegemea upande mmoja wa kumkandia Manji..au umetumwa na huyo unayemwita ''mtoto wa kigogo'' nn? Acha Usimba ww!!

    ReplyDelete
  13. Wanachama wa Yanga wameshazoea dezodezo,kupewa hela nyingi then hawako accountable wala responsible...soka saiv limebadilika inabidi wapewe elimu jinsi gani soka linavoendeshwa kama wanataka yanga siku moja ikue...kama wanaogopa bl 3 hapo kuna maendeleo hiyo inaonesha kuwa ni wavivu hawataki kukaa chini kupanga maendeleo ya timu wao wanataka mtu tu awe anatoa hela wajinga wazitumie halafu hakuna maendeleo yoyote...hata wewe shaffih ungekuwa Manji unatoa hela tu hauoni maendeleo...na wewe ungekuwa joyful basi ungekewa hauna akili ya Maendeleo....mimi naamini kabisa unaelewa how modern soccer is supposed to be managed,toa elimu hiyo kwa watu na ushawishi mkubwa unao...vilabu vyetu vinavyoendeshwa hatufiki popote nakuambia mapinduzi yanahitajika katika soka kila siku tushabikie Arsenal,man u au Barca inabidi tujifunze how did they manage to reach there na soka bila kuendeshwa kibiashara kwa ulimwengu huu sijui tz tutabaki mkiani all the time...wanachama wa yanga wanapaswa kuacha uvivu,wachukue risk kama hawamtaki Manji basi wakakope hela bank waendeshe timu kibiashara adabu ya fedha itakuja tu wakiona wana deni bank la sivyo basi ndo watakuwa wanachimbia kaburi klabu yao...ama wabaki kushinania kombe la mil 30 fedha ambazo si kitu kwa klabu

    ReplyDelete
  14. WE SHAFFIH TUACHE NA YANGA YETU,TUTAKUPOTEZA....TUTAKUMALIZA KUMBUKA HAKUNA MTU ANAKULINDA.

    ReplyDelete
  15. Another poor shaffih experience,hivi utabadilika lini?

    ReplyDelete
  16. Shaffih waTanzania tuna upeo mdogo wa akili baadhi yetu, ndio maana Magazeti huwa yanatuchezea sana,Yanga ya safarihii ni ya Afrika, Simba hii wee acha tu, tunapenda kuambiwa ujinga ujinga ndio tunafurahi, Mimi nafurahi Manji kuichukuwa Yanga najua nia yake kubwa ni kuifanya kuwa klabu kubwa Afrika, lakini wanaYanga wajue Kama wakimpitisha na Hao jamaa zake magari na kleb basi wajue Yanga inaangukia mikononi maw Manji!, kimaendeleo ya soka ni vizuri iwe hivyo na nataka klabu zote mbili zipate watu wa namna ya Manji klabu itoke kwenye kumilikiwa na Wanachama (Akilimali) iwe ya mtu mmoja ambaye ataweza kuimeneji na kuindesha kibiashara , mimi nataka hizi klabu zisiwe na wanachama kabisa, zikiwa hivyo basi Yanga na Simba zinakuwa na maendeleo kuliko hata Azam , kwanini tusiwe washabiki au wapenzi Kama tunavyoshabikia Manchester , Arsenal ......... Kunawatu wanajiita Yanga na Simba lakini uwanjani wanaingia bure ! Hapo patakuwa na maendeleo kweli HUU NI UZALENDOOO!!! yani Yule jamaa ndio muwakilishi wanayanga na Simba aslimia 80 ya wanachama wako dizaini ile ushamba ushamba!! Ninahakika Manji ataimiliki Yanga jumlajumla hapo baadae MUNGU amsaidie ili soka likuwe Kama unavyopenda Shafii mwache atupeleke kile tunapotaka ukila na kipofu usimshike mkono Hilo ni pigo kwa wale njaa wanaotaka kuishi kwa kuitumia Yanga na maendeleo kwa kuelekea kwenye soka la ukweli. Mohd Omar Elhind dsm bigup shaffiih Dauda nakuaminia japo jamaa hawakuelewi, lakini tutafika.

    ReplyDelete
  17. Shaffi hapo umesema kweli

    ReplyDelete
  18. Inakuuma mtu mwenye pesa/malengo na Yanga kuamua kuongoza Club. You are a Simba supporter we know that for fact. Na hao anti Manji nimewasikia kwako tuu no where else. Hata Nabii hakubaliki kwao. Sasa cheki hizo comments, kuna Anti manji hata 1 ??? Lierrrrrr !!!!

    ReplyDelete
  19. Huyo ndo mchambuz wa soka bhaana! Utumbo m2pu

    ReplyDelete
  20. Huyo ndo shafii! Utumbo m2pu

    ReplyDelete
  21. Naomba kuuliza,kwani wewe(Shaffih)umetumwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna ubishi jamaa anapotosha mno! Tena co soka la bongo 2 ata ulaya, ye anadhan wote tunamckilza yy 2 bila kufuatilia kwenye mitandao

      Delete
  22. Tangu lini mtu akakupa kitu bure! Wanayanga fikirini manji analipa mishahara ya makocha na wachezaji toka mfuko gani?? Ndio muanze kuandika matusi! Shafii anajaribu kutoa facts nyie mnamtukana hivi kuna mtu atatoa pesa yake bila kupata chochote? Kueni kimawazo!!!

    ReplyDelete
  23. SASA NAANZA KUHISI HATA WAANDISHI WA HABARI MNAPOTOSHA UMMA KUHUSU MAENDELEAO YA SOKA...SHAFIII UMEWAHOJI HAO WANOJIITA MA ANTI-MANJI KUWA WANADHANI SHEHE MANSOUR ANAMILIKI MAN CITY KWA FAIDA YA NANI KAMA SIYO BIASHARA ZAKE AT THE SAME TIME TIMU INAENDELEA SASA WAO WANATAKA MANJI ATOE HELA YAKUENDELEZA TIMU KAMA SADAKA KANISANI AU MSIKTINI...HATA ANAYETOA SADAKA ANATARAJIA KUPATA BARAKA TOKA KWA MUNGU.
    KWA UPANDE WANGU MIMI MPENZI NA SHABIKI WA YANGA NAUNGA MKONO JUHUDI ZA KUBINAFSISHA TIMU KWANI MWISHO WA SIKU MASHABIKI NA WANAHISA WATAKUWA NA HAKI KWA NAFASI ZAO TOFAUTI HUONI ENGLAND KUNA CHAMA CHA WAPENZI WA MPIRA NI SWALA LA SATISFACTION NA SATISFACTION INA MIPAKA KAKA SHAFII. WALIOKUELZA AU KAMA UMEAMUA KUANDIKA KWA MATAKWA YAKO NI UPOTOSHAJI HASA KWA SISI TUNAOONA SOKA LA SASA NI ZAIDI YA USHABIKI NI BIASHARA ZAIDI.....HAO WANAJIITA WANACHAMA MA ANTI-MANJI MBONA HAWATAKI KUTAJA MAJINA YAO..? WAKINA AKILI MALI WALIKUWA ANTI UONGOZI WALIKUWA HAWAJIFICHI WALIJITOKEZA WAZI WAZI.....TUACHE SOKA LA USHABIKI TUENDE KWENYE SOKA LA KIBIAHSRA NA USHINDI NDIPO TIMU NA SOKA LA TZ LITAENDELEA.........YANGA ITAKAPO BINAFSISHWA NITAKUWA MTU WA KWANZA KUNUNUA HISA HATA KWA MKOPO WA BENKI....

    ReplyDelete
  24. kaka shaffih hakuna mtu ambae anasoma blog yako karibia kila baada ya lisaa limoja kama mm!kuutambua upeo wa mtu mjinga ni rahisi sana kuliko kuutambua upeo wa mtu mwerevu na msomi!yanga kama yanga ni mali ya wanachama tunaomba usijaribu kuupotosha umma na wanayanga kwa ujumla!hesima yako kwa jamii ilikua kubwa sana ww na eddo kumwembe kutokana na usimba unaouleta katika blog yako mpaka eddo amekukimbia na gazeti lenu la number 10 limekufa kwa ufupi kaka mpira haujui umejaa ubishi ushamba na majungu ya kuleta usimba na uyanga hadi clouds fm na tv.ulikua na mtu mwelevu eddo mpaka mkasimamisha number 10 ameondoka umebaki ww peke yako umeshindwa kujiendesha kutokana na mawazo yako mgando na finyu!hakuna cha anti manji wala shangazi mansour tunakuomba tuachie yanga yetu haikuhusu kama vipi usiandike habari za yanga kwenye blog yako huyo mtoto wa kigogo ni nani?tunawahitaji hao anti manji uwaweke hadharani tuwajue wasioitakia mema na maendeleo ya yanga!nimekusikia jana redion kwenu mkilichambua suala la yondani na nikapitia blogy yako ulichokiandika ni ujinga mtupu mpaka ukatumiwa msg toka texas kua yondani ndio mtu atakae kua liable lakini ww umelishupalia utafikiri yondani mdogo wako haya watu wamekutumia picha sema!kuna ishu ya jeba ingekua yanga ndio wamefanya vile kwa azam ungeandika na kupamba ila kwasababu simba ndio wanahusika umekaa kimya!tumeichoka blog yako kaka badilika saidia mpira wa Tanzania usonge mbele!mpira wa bongo bila akina manji hautasonga muite utakavyomuita Manji ndio mtu sahihi tunaemtaka Wanayanga hao ma anti manji waambie wakaanzishe club yao kwani lazma kua mwanchama wa yanga?si waanzishe club yao wasisaidiwe na manji?kipi wanachokililia yanga au wameisaidia nn yanga izo mali za yanga zinawahusu nn wao?andika hoja za msingi kaka la sivyo blog yako itakosa wasomaji kila la kheri!nakukumbusha tu tunahitaji zile clips ulizotuahidi za wachezaji wa kitanzania wanaoishi sweden stay tuneeeedddd mpaka leo?acha ubabahishaji kaka!

    ReplyDelete
  25. KAKA SHAFII PAMOJA NA SAFARI ZOOTE ZA ULAYA ULIZOKKUWA UNATUSIMULIA HUJAELIMIKA NA KUKOMBOLEWA......DO POLE SANA KWELI UBINADAMU KAZI NA INAONYESHA JINSI GANI TUNA SAFARI NDEFU YAKUJIKOMBOA KIFIKRA KWA WATU WENGI.....

    ReplyDelete
  26. kaka shaffih mi nakushauri ungewaachia wanayanga waamue wenyewe,najua wana akili timamu na mazuri na mabaya ya manji wao ndio wanayajua,usijitafutie ubaya kwenye hili ona sasa wanavyokusema?waache yanga waamue wenyewe mambo yao kaka.

    ReplyDelete
  27. Ivi nyinyi mnaacha kujibu hoja mna m attack shaffih nyinyi vp nyinyi?nani mwerevu hapa?anayeacha meseji hewani afta approval au anayeandika matusi??kama hutaki hoja jibu hoja sio shaffih.kama mnaona ana usimba nendeni blog zingine leo iwe mwisho apa.tatizo wabongo ukiigusa 2 yanga wanakutajia ata maisha yako.sasa eti ulaya ooh number 10 ooh shaffih hujaelimika?KAMTISHENI MTOTO MDOGO.HUU NDO UHURU WA HABARI.KAMA VP MSISOME HII BLOG.WAPENZI WAPO WENG SANA.

    ReplyDelete
  28. WEWE ANNONYMOUS HAPO JUU UHURU PASIPO MIPAKA NI UTUMWA.......SHAFII KAMA MWANAHABARI ANAGEPATA PIA NA MAWAZO YA WALE WANAOUNGA MKONO MANJI KUWA KIONGOZI YANGA MBONA HAJAWAHOJI...?
    BINAFSI SIPINGI MAWAZO YA SHAFII BUT HE IS SUPPOSED TO BE VERY OBJECTIVE AND EVIDENCE AND FACT ORIENTED SPORTS JOURNALIST.......UKISOMA KWA UMAKINI NA KUCHAMBUA KWA KINA HIYO HABARI NZIMA IMEJAA USHABIKI NA UNAZI...NA SASA ONA ALIVYOTUMA MARA YA PILI MKATABA WA YONDANI NA SIMBA WHT I EXPECTED JIONIHII ANGETULETA MAHOJIANO YAKE NA YONDANI....VIONGOZI WA SIMBA PAMOJA NA YANGA TUNGEJUA VIEWS ZAO....SHAFII USIWE THAT MUCH BIASED JOURNALIST...

    ReplyDelete
  29. Shafii mnamshangaa leo jamani! Huyo ndivyo alivyo! Walimtoa Maximo kwa majungu ya kiswahili mimi sitowasahau. Mchambuzi wa soka sahihi Tanzania ni mmoja tu, Eddo peke yake, mchambuzi wa soka ukimsikiliza hutakiwi kugundua ana mapenzi na timu gani kwa muda mfupi kama waandishi wa aina ya Shaffi.

    ReplyDelete