"Kushinda vizuri michuano kama hii ni lazima ukutane na timu kubwa na nzuri katika hatua fulani. Michuano ya Euro ni ya kiwango cha juu, hivyo sitegemei kupata ushindi kirahisi. Kwa kuanza tu tutakutana na Ureno na Uholanzi na nategemea kwamba tutakuwa tayari kupambana na kupata matokeo. Hii ndio nguzo ya timu yangu."
Qn: Timu gani inayokutisha?
"Majina yale yale ya kila siku, Spain, Uholanzi, waitaliano na labda Ufaransa.Qn: Kuna matumaini makubwa kwamba Ujerumani watafanikiwa kubeba taji mwaka huu. Unadhani kuna ukweli ndani yake?
"Unapoangalia performance yetu nzuri kwenye michuano ya WOZA 2010 na kwenye hatua ya kufuzu ya michuano hii, hatuna budi kujiamni kwamba tunaweza kushinda taji hili. Sapin bado ndio timu ambayo tunapaswa kuishinda, lakini naamini tupo njiani kuwakamata. Ni imani yetu tunaweza kufanya makubwa ikiwa tutacheza kwa kujituma na kuepeuka balaa la majeruhi, chochote tunaweza."Qn: Kitu gani kinachokufanya kuwa imani kubwa hivyo?
"Ubora wetu wa kucheza soka na uwezo mkubwa wa kufunga magoli tulionao kwenye timu. Tuna uwezo mkubwa wa kushambulia na kukaba, pia tuna umoja sana miongoni mwetu,. Tunapenda kuwa pamoja kwa ajili ya kulipigania taifa letu na jambo hilo linatufarahisha sana kuitetea heshima ya nchi yetu."Qn: Kwa sasa wewe ni mmoja ya washambuliaji wenye rekodi nzuri duniani kwa upande wa klabu na timu ya taifa. Unaliezeaje form yako hii uliyonayo?
"Yote yanwezekana na kujifunza zaidi kwenye mazoezi, kujifunza zaidi na kujaribu kuboresha kila kipengele cha mchezo wangu na pia kutokuridhika. Kwa miaka 26 niliyonayo, nipo kwenye umri sahihi kabisa kwa mshambuliaji. Nina uzoefu na sina tena ile hali ya kusumbuliwa na makosa niliyoyafanya kwa kupoteza nafasi, sasa hivi nimetulia zaidi na kugeuza makosa yangu yaliyopita kama changamoto ambazo natakiwa kuzifanyia kazi. Ni hali ya kujitambua zaidi."Qn: Upo vipi upinzani wako na Miroslave Klose kwenye kupata nafasi ya kuongoza mashambulizi?
"Usindani ni sehemu ya mchezo. Inabidi kukubaliana na hilo, jifunze kupitia hilo. Miro ni mfungaji hatari sana, amefanya maajabu kwenye timu ya taifa kwa kipindi kirefu sana. Ushindani kati yetu ni mkali sana na weney heshimandani yake, lakini ni vita ya kuvutia. Na mwenye ubora zaidi atashinda. Ninachoweza kusema kama nikiwa fiti na kuendelea kufunga, basi utabaki kuwa ni uamuzi wa kocha."Qn: Nini kilichokusuma na kukutia nguvu wakati ulipokuwa hufungi mabao kwa nchi yako?
"Hijawahi kuwa rahisi kuvumilia kuzomewa na kuulizwa na watu tofauti ni vipi unashindwa kufunga mabao kwa nchi yako kama ufanyavyo kwa klabu yako. Siku zote nilikuwa najua na kuwa na imani na uwezo wangu, hivyo nikawa na lengo wa kuwathibitishia waliokuwa na mashaka na uwezo wangu. Hilo ndilo lilonisukuma zaidi, namshukuru sana kocha wangu hapa Joachim Low. Wakati wengi wakisema na kutabiri kwamba sitofanikiwa kama mshambuliaji wa kimataifa, yeye aliendelea kuwa na imani na mimi na kuniambia niendelee kusonga mbele. Aliponipa unahodha kwenye mechi dhidi ya Ukraine mwaka jana alinitimizia ndoto yangu ua utotoni, ukizingati ailikuwa ndio mechi yangu ya 50 kwa taifa langu. Hilo jambo lilinisukuma sana na pia lilionyesha umuhimu wangu kwenye timuya taifa. Baada ya matatizo yote nilijihisi nimezaliwa upya."
No comments:
Post a Comment