Kama kocha wa zamani wa England alivyosema: "Nusu ya kwanza nzuri, na nusu ya pili sio nzuri sana."Baada ya kufuzu vizuri, mipango ya Euro kwa England iliingia kirusi mwezi February baada ya kocha Fabio Capello kujiuzulu huku FA wakichelewa kumtaja mrithi wake.
Wiki sita kabla ya fainali za Euro kuanza, Chama cha soka cha nchi hiyo kilikuwa kinakaribia kumteua Roy Hodgson kama manager. Hali ya kutokueleweka kwenye benchi la ufundi iliongeza tu idadi ya matatizo ya England, ambayo yalimuhusisha mshambuliaji wa kutumainiwa, Wayne Rooney, ambaye alikuwa amesimamishwakwenye mechi zake mbili za ufunguzi wa michuano hiyo; na tumaini lao kubwa kwenye kiungo, Jack Wilshare alikuwa tayari ameshaondolewa kwenye ratiba za michuano hiyo kutokana na majeruhi.
Mashabiki wakaonyesha kukata tamaa kwa kuzibania wallets zao, wakinunua tiketi nusu ya 6000 walizowekewa hasa kwa mchezo wao dhidi ya Ufaransa mjini Donetsk. Wakati gharama za usafiri na hotel nchini Ukraine zikiwa moja ya sababu, ukosefu wa hamsha hamsha ambayo siku zote waingereza na mashabiki wao wanakuwaga nayo ilionyesha kiasi gani kwamba hata washabiki vyombo vya habari na hata mashabiki wameshaona nafasi ya kufanya vizuri kwa timu yao ilivyo ndogo.
Mwamko huu hasi unaweza ukawa umechangia kwa Capello, kuonekana kwenye kituo cha TV nchini Italia akiwasema FA ya uamuzi wao wa kumvua unahodha John Terry baada ya mlinzi huyo kutuhumiwa kumtukana kibaguzi Anton Ferdinand wakati wa mechi ya EPL. Mwenyekiti wa FA David Bernstein akaamua ku-demand kuondoka kwa Capello.
Mahusiano baina ya Capello na watu wengi muhimu wa soka la kiingereza, zikiwemo media na makocha wa vilabu ulifikia hatua mbaya mpaka kuvunjika. Mzozo wa Terry uliwapa FA na Capello njia rahisi ya kuondokana na mkataba wa £6million kwa mwaka.
Kufuatiwa kuondoka kwa Capello, FA wakakataa kufanya haraka ya kumuajiri kocha mpya, msaidizi wa Capello Staurt Pearce, ambaye tayari alishakuwa kocha kamili wa kikosi cha Great Britain kwa ajili ya Olympic na kikosi cha vijana wa under-21, akawekwa kama kiraka.
Kocha wa Tottenham Harry Redknapp alikuwa ndio chaguo la wengi, lakini form mbaya Spurs kuelekea mwishoni mwa msimu baada ya kuhusishwa na kazi ya ukocha England ikawafanya FA wabadili mawazo na kumuona Hodgson kama mtu sahihi, na pia FA hawakuwa tayari kuwalipa Tottenham mamilioni ya paundi kama fidia ya kumchukua Harry.
Badala yake wakamchukua Hodgson ambaye alikuwa nje ya mkataba na West Bromwich Albion, na kumaanisha FA watatumia kiasi kidogo kupata huduma zake. Hodgson akateuliwa kuwa kocha mpya na siku kadhaa baadae akatangaza kikosi chake huku akimaliza utata uliokuwepo ni namna gani Rio Ferdinand angekaa vipi chumba kimoja na John Terry, kwa kuamua kumuacha veteran wa Manchester United.
Wakati kukiwa kumebakiwa takribani wiki mbili ya kick off ya Euro England wakaanza kupata majeruhi, wa kwanza alikuwa Gareth Barry, Frank Lampard akafuata na jana jumapili Gary Cahil nae ameondolewa kwenye kikosi, huku John Terry na kiungo tegemeo Scott Parker wakiwa na mashaka matupu juu ya ufiti wao wa kucheza Euro 2012, hivyo kuzidi kuiacha England ikiwa na hali mbaya.
Pia ikumbukwe vijana wa Hodgson inabidi wacheze mechi zao mbili za kwanza dhidi ya France na Sweden bila mshambuliaji wao tegemeo Wayne Rooney mwenye adhabu. Roy amejaribu kutafuta suluhisho kwenye mechi mbili za majaribio ambazo amepata matokeo ya ushindi wa 1-0 kwa kila mechi, lakini bado England inaonekana kutotisha kwenye safu ya ushambuliaji bila Wazza, tena ikizingatiwa atakosekana kwenye mechi ngumu zaidi.
Kwa jinsi hali halisi ilivyo kwa mara ya kwanza Waingereza wakiongozwa na vyombo vyao habari ambao siku zote wamekuwa wakishindwa kuwa wakweli juu ya ubora wa timu yao, safari hii kwenye Euro wote wameonekana kuwa kimya bila kuwa na matumaini makubwa.
Hata mie sioni namna England watakavyofanya vizuri kwa michuano hii labda ijitokeze miujiza ya soka kama iliyotokea mwaka 1992 ilivyotokea kwa Denmark.
Utabiri: Kuvuka hatua ya makundi ni mafanikio makubwa sana kwa England kwenye EURO 2012.
RATIBA YA MECHI ZAO
Group D
11.06.12 France (Donetsk, Ukr)
15.06.12 Sweden (Kiev, Ukr)
19.06.12 Ukraine (Donetsk, Ukr)
Group D
11.06.12 France (Donetsk, Ukr)
15.06.12 Sweden (Kiev, Ukr)
19.06.12 Ukraine (Donetsk, Ukr)
No comments:
Post a Comment