Wawakilishi wa Rio Ferdinand leo wameonekana kuchukizwa na kitendo cha Roy Hodgson kutomuita kwenye kikosi cha England mteja wao baada ya Gary Cahil kuondolewa kwenye kikosi kutokana na kupawa na majeruhi.
Chama cha soka cha England kilithibitisha Jumapili ya leo kwamba Gary Cahil ameondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kuumia kwenye mechi dhidi ya Ubelgiji.
Huku watu wengi wakitegemea Roy Hodgson angemuita Rio kuziba pengop la Cahil, kocha huyo badala yake amemuita mchezaji kinda wa Liverpool Martin Kelly, ambaye alicheza mechi yake ya kimataifa alipoingia kama sub kwenye mchezo dhidi ya Norway.

Jamie Moralee |
Na jambo hilo limeonekana kuikera kambi ya Ferdinand ambao wamesema kuna jambo lingine zaidi ya "sababu za kisoka" alizozitaja Hodgson alipomtema Ferdinand kwenye kikosi chake cha kwanza.
Mwakilishi wa Ferdinand na rafiki wa siku nyingi wa mchezaji huyo Jamie Moralee: "Lampard,Terry, Barry, Gerrard; wote wana umri mkubwa lakini wameitwa kwenda Euro. Kwanini iwe kwa Ferdinand tu?
"Kumtendea hivi mchezaji ambaye ameshaiongoza timu ya taifa na kuichezea mechi zaidi ya 80, ni ukosefu wa heshima kutoka kwa Hodgson na FA kwa ujumla."
Kwa upande wa mchezaji mwenyewe Rio Ferdinand aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: "Kwa sababu zipi???????"
No comments:
Post a Comment