Search This Blog

Saturday, June 2, 2012

EXCLUSIVE INTERVIEW NA KOCHA WA UJERUMANI: TIMU YANGU INA NJAA NA MACHO YOTE TUMEWEKA KWENYE LENGO LA KUTWAA EURO 2012

Katika kuelekea michuano ya EURO 2012, nilitafuta nafasi ya kuonana na kocha wa timu wa timu ya taifa ya Ujerumani nikiwa nchini humo nilipoenda kwa madhumuni ya kuangalia fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya. Nilifanikiwa kuonana na Joachim pamoja na mchezaji Mario Gomez na kufanya mahojiano kuhusu michuano ya Euro 2012 na nafasi ya Ujerumani kwenye Michuano hii.
Kwa kuanzia tuanze na interview na kocha Low na ilikuwa kama ifuatavyo.


Shaffih: Unajisikiaje kupangwa kwenye group ambalo wengi wanaliita kundi la kifo?

Low: Kwa sura ya kundi, tumepangwa kwenye kundi ngumu zaidi kuliko yote. Uholanzi na Portugal  zote ni timu zenye wachezaji wa daraja la dunia na mechi zao dhidi yetu zitakuwa ni ngumu sana; nadiriki kusema mechi kufa na kupona. Kwa upande wa Denmark, kwa miaka kadhaa wameshaonyesha kwamba wanaweza kushindana kwenye michuano mikubwa. Hawaogopi timu zenye majina makubwa na hawana cha kupoteza na hilo linawafanya wawe hatari zaidi na wasiotabirika. Kwa maana hiyo nasema kwamba kila timu kwenye kundi B ina nafasi ya kupita.



Shaffih: Mliwamaliza na kuwazidi kwa kila kitu Uholanzi kwenye mechi ushindi wa 3-0 mwezi November. Hilo linakupa nguvu yoyote kisaikolojia?

Low: Usiku ule tulicheza soka la aina yake na la kipekee na ndio maana tukapata matokeo chanya kutoka mchezo ule. Uholanzi tutakayokutana nayo kwenye Euro itakuwa na nguvu zaidi na yenye kubadilika sana hilo nina uhakika.



Shaffih: Je rekodi yenu nzuri kwenye hatua ya kufuzu inaweza kuwaletea matatizo yoyote kwa maana ya wachezaji kujiamini sana?
Low: Sina wasiwasi kabisa kwenye matokeo yale. Kikosi nilichonacho kina njaa ya mafanikio, na kipo focused  kwenye lengo la kushinda kikombe. Hakuna aliye kwenye fikra kama tulimaliza kazi kwenye kufuzu tu japokuwa tulifanya vizuri sana.


Shaffih: Ujerumani wanaangaliwa kama moja ya timu zinazopewa nafasi sana na imani ipo juu hapa Ujerumani kwamba mnaweza kubeba kombe . . .
Low: Baada ya kufanya vizuri kwenye kufuzu, mategemeo yamepitiliza. Lakini droo ya kundi tulilopangwa kidogo imeshusha mategemeo. Sasa watu wanaangalia hali halisi kidogo. Lolote linaweza kutokea kwenye michuano. Majeruhi yanaweza yakabadilisha kila kitu. Kama makocha wengine, nitakuwa naomba tuepukane na balaa hilo na tumalize michuano tukiwa tuo salama ili kuweza kukamilisha ndoto ya ubingwa wa Euro 2012.


Shaffih: Nini nguvu yenu?
Low: Moja ya vitu vikubwa kwangu mimi ni kuona namna tulivyojimaarisha na kuendelea kuja kuwa timu ya ukweli, ambayo ina umoja ambao ndio nguzo yetu. Hakuna mchezaji ambaye moja kwa moja anajiangalia yeye. Kila mmoja wetu anamsaidia mwenzake, tunashirikiana kuiletea mafanikio timu yetu, na pale vijana wapya wanapokuja wanakuta mfumo huo na kuumudu vizuri. Spirit ya timu ilikuwa juu sana kwenye WOZA 2010 PALE South Africa  na hili limeendelea mpaka leo.


Shaffih: Je Euro 2012 inaweza ikawa vita ya kwenu pamoja na Spain?
Low: Spain wapo vizuri sana lakini sio kama ndio wagombea taji pekee. Uholanzi na timu nzuri sana. Siku zote nimekuwa na heshima kubwa juu ya uwezo wa Ureno, France wanaimarika, na tusiwatoe England..


4 comments:

  1. No, no, tupe ushahidi hii ya kusema umefanya interview na kocha wa Ujerumani na Gomez bila video clip...

    ReplyDelete
  2. Shaffih tafadhali bwana weka picha au video clip tuone ili tujiridhishe kufanya interview na Loew au Gomez sio kitu kidogo tu kwako hata media za Germany ni issue,so ukiweka evidence itakuongezea credit kwako na media house yenu.

    ReplyDelete
  3. without disrespect you pls mr shaffy hebu tuwekee tu hata picha ya still kama kweli umeonana nae.na kama huna unajishushia hadhi,there is no need for that.



    OCD

    ReplyDelete
  4. aisee wadau acheni ushamba picha ya nini ? au hamjui kama Shaffih alikua ulaya for about two weeks ? sasa mnataka picha za nini ? acheni mambo ya kishamba hayo,mmeona interview ngapi kwenye mitandao mbali mbali bila ya hizo picha mnazozitaka ? acheni hizo, kukutana na Joachim Low na Mario Gomez hasa ukiwa ulaya si kitu cha ajabu kwasababu nao pia wanadamu wanatembea, inawezekana alikuatana nao bar au kwenye mgahawa au mtaani tu, hapo hakuna cha ajabu inategemea unapokutana na mastaa ghafla unataka nini,tulio wengi tukikutana nao tunataka kupiga picha lakini shaffih kama mwandishi wa habari za michezo kwake priority siyo picha zaidi ya kutaka kufanya interview ya haraka,mfano mimi niliwahi kwenda hotel ya hayatt nchini Afrika ya kusini nikakutana na Eric Cantona kwa bahati mbaya, nikamuuliza kwa nini aliamua kustaafu soka ghafla. akaniambia ni kwasababu hakutaka malumbano kwani kutokana na mashabiki kupenda matusi angewapiga na mwisho wa siku angeishia kufungiwa kwaiyo akaona bora aachane na soka ili afuatilie mambo mengine,ilikua ni kwa bahati mbaya kukutana na Cantona na sikua na Camera wala chochote,

    ReplyDelete