Baada ya kuwa michuano mibovu zaidi kwenye Euro 2000, ambapo walishindwa kushinda hata mechi moja na hatimaye kutolewa kwa aibu kabisa kwenye raundi ya kwanza - lakini mabadiliko yaliyofanywa kuubadilisha mfumo wa maendeleo ya soka la vijana, taratibu taratibu, umerudisha soka la Ujerumani kwenye hadhi yake. Na mashabiki wameamini kwamba kikosi cha sasa kinachoundwa na vijana zaidi ni mwanzo tu wa safari ya kuelekea kubeba taji lao kwanza toka EURO 96.
Utafiti uliofanywa na jarida maarufu nchini humo (Kicker) unaonyesha zaidi ya 2/3 ya watu waliohojiwa wanategemea nahodha wao Phillip Lahm atabeba kombe mjini Kiev, July 1, huku wakiamini wachezaji kiungo mchezeshaji Mesut Ozil na mshambuliaji Miroslave Klose watakuwa na tuzo mchezaji bora wa mashindano na mfungaji bora.
Ujeumani wamepangwa kwenye kundi ambalo wengi wanaliita la kifo - watacheza mechi zao tatu za mwanzo dhidi ya Ureno, Uholanzi na Denmark, na wachambuzi wengi wengi wa soka wamekuwa tu hawawapi nafasi ya kuvuka kwenye hatua ya makundi bali pia wanapewa nafasi kubwa ya kubeba kombe hili mwisho wa michuano hii. Wakiwa na kikosi cha vijana kabisa chenye wastani wa umri wa miaka 24 - ambacho ndio kikosi chenye wachezaji vijana zaidi waliowiva zaidi tangu mwaka 1934. Klose, Ozil, Mario Gomez, Thomas Muller na Lukas Podolski wataunda safu ya ushambuliaji ya kutisha zaidi kama tulivyoona kwenye WOZA 2010. Huku Manuel Neur akiiongoza safu bora ya ulinzi inayoundwa pia na Holger Badstuber, Boateng, Hummels na nahodha Lahm, Mario Gotze, Khedira, Toni Kroos na Bastian Schweinsteiger wakiunda safu bora kabisa ya kiungo.
Hawa ni vijana wenye umri mdogo lakini wamekamilika na wana uzoefu mkubwa, wana uwezo wa kucheza timu yoyote wakiwa hawana woga na wala mashaka yoyote juu ya kujitoa kwa nchi yao - huku nyuma yao wakiwa na umati wa mamilioni ya mashabiki wa Ujerumani ambao wote wana imani kubwa sana juu yao. Tegemea makubwa kutoka vijana wa Joachim Low kwenye michuano hii.
MAPINDUZI YA STAILI YA UCHEZAJI
Kitu kingine ambacho Ujerumani walichonacho kwenye timu, ni aina ya mchezo uliosukwa vizuri kiakili zaidi na management ya Low. Katika miaka 6 aliyokaa kwenye benchi la timu ameleta mapinduzi makubwa ya uchezaji wa soka la kuvutia na ushindi tofauti na vikosi vya nyuma vilivyokuwa vikicheza la moja kwa moja na kushinda kwa vyovyote vile.Ujerumani sasa inacheza soka la kuvutia na kushinda mechi kwa magoli mengi ya kiufundi zaidi, na ndio maana haikushangaza pale Bosi wa timu ya taifa ya Spain Vicente Del Bosque alipowaelezea kama ndio "kikosi cha Ujerumani kinachocheza zuri zaidi" ambacho Del Bosque amewahi kukishuhudia kwenye maisha yake.
KUNDI LA B ILIPO UJERUMANI EURO 2012
Team | Pld | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Netherlands | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
Denmark | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
Germany | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
Portugal | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
RATIBA | ||
---|---|---|
9 June 2012 | ||
Netherlands | Match 3 | Denmark |
Germany | Match 4 | Portugal |
13 June 2012 | ||
Denmark | Match 11 | Portugal |
Netherlands | Match 12 | Germany |
17 June 2012 | ||
Portugal | Match 19 | Netherlands |
Denmark | Match 20 | Germany |
UJERUMANI ILIFIKAJE KWENYE EURO 2012
|
No comments:
Post a Comment