Search This Blog

Saturday, June 2, 2012

LIVE MATCH CENTRE: TANZANIA 0 - 2 IVORY COAST FULL TIME



DK 90: Ivory Coast 2-0 Tanzania
DK 86: Goaaaaaaaal Ivory Coast wanapata bao la pili na si mwingine ni Didier Drogba.
DK 80: Kipindi cha pili kinaelekea mwishoni na bado Tembo wanaoongoza kwa bao 1-0
DK 75: Matokeo bado ni 1-0, Ivory Coast wanaongoza.
DK 70: Aggrey Morris anapata kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

DK 68: Ivory Coast 1-0 Tanzania
DK 60: Ivory Coast 1-0 Tanzania
Second Half: Kipindi cha pili kimeanza
Half Time:  Ivory Coast 1-0 Tanzania

DK 43: Ivory Coast 1-0 Tanzania

DK: 24 - Solomon Kalou anaipatia goli la kuongoza Ivory Coast



Kocha Kim Poulsen ametaja kikosi cha Taifa Stars ambacho leo (Juni 2 mwaka huu) kitakuwa uwanjani kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan kuivaa Ivory Coast katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.
Amefanya mabadiliko katika nafasi mbili kwenye kikosi ambacho Mei 26 mwaka huu kilicheza mechi ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu.
Amir Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho Ngasa atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. Ngasa atacheza nafasi ya Haruna Moshi ambaye hayuko na Stars hapa baada ya kuumia mazoezini siku moja kabla ya safari.
Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;
Kipa; Juma Kaseja
Mabeki; Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani
Viungo; Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto
Washambuliaji; Mbwana Samata na Mrisho Ngasa
Wachezaji wa akiba; Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano.
Kim amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).
Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani.
Mwamuzi; Slim Jedidi (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba 1; Bechir Hassani (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba mbili; Sherif Hassan (Misri)
Mwamuzi wa akiba; Youssef Essrayri (Tunisia)
Mtathmini wa waamuzi; Rachid Medjiba (Algeria)
Kamishna wa mchezo; Saleh Issa Mahamat (Chad)

7 comments:

  1. Al th best taifa stars

    ReplyDelete
  2. mechi ni saa ngapi

    ReplyDelete
  3. Justine Rugaimukamu JBRJune 2, 2012 at 9:15 PM

    Taarifa zinakosea,hatuwezikufungwa na watu kama Drogba,Kalou nk.Jembeletu Juma Kaseja alishatuhakikishia ushindi kabla ya mechi!!!!

    ReplyDelete
  4. acha uzushi shaffih...kufunga na kufungwa ni jambo la kawaida kama zambia waliweza..isiwe kwa Tanzania,be considerate on your final statements,tunakupenda sana so please don even let chance to people to start hating you,let wisdom prevail...

    ReplyDelete
  5. wabongo hatuna uzalendo,mechi ya tz vs ivory coast haioneshwi bali za mbele huko zinaoneshwa,tutafika kweli!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. nafatilia sana comment zako brother shafii naungana na wewe mia kwa mia tutengeneze national team walau kwa miaka 5,kwa sasa tunajidanganyana kama tuna tegemea kufuzu,match hizi ziwe kama za kuwapa uzoefu vijana
    watu kama nyinyi shafii ndio mnafaa kwenye medani ya soccer
    jamani tubadilike kwa sasa hata national team apewe guardiola NI KAZI BURE
    PESA ZINAZOTUMIKA SASA HIFI NI BORA TFF INGEWEKEZA KWENYE KUTENGENEZA TIMU NZURI YA VIJANA WALAU KWA MIAKA 5 THEN TUINGIE NAYO MASHINDANONI HAPO NAAMINI TUTAPIGA HATUA LAKINI SI KWA SASA,NI KUCHEZEA PESA TU NAULI KWENDA KURUDI POSHO MNATUBOA JAMANIII

    ReplyDelete