Uzoefu mara nyingi ni muhimu sana katika michuano mikubwa na UEFA EURO 2012 kutakuwepo na wachezaji wasiopungua 12 ambao wameshacheza mechi zaidi ya 100 - huku kukiwa kuna wengine wakiwa wanakaribia kufikia idadi hiyo ya mechi.
Wakati kukiwa na mengi ya kuzungumza kuhusu vipaji vya wachezaji wachanga, uzoefu unaweza ukawa na umuhimu katika michuano mikubwa. Wachezaji ambao wameshajifunza vitu vingi na kukabiliana na presha ya mechi kubwa kwa mara nyingi zaidi wana uthamani mkubwa kwa timu yoyote, na watakuwepo wachezaji namna hiyo wengi wakiuleta uzoefu wao kwenye michuano ya Euro 2012.
Wanaume 12 watasafiri kwenda Poland na Ukraine huku wakiwa na uzoefu wa kucheza mechi zaidi ya 100, in fact, huku Spain's goalkeeper Iker Casillas akiwa anaongoza listi hiyo kwa kucheza mechi 130 akiwa na mabingwa wa ulaya na dunia. Kipa wa Real Madrid alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Sweden miaka 12 iliyopita na akaweka rekodi mpya Jumatano iliyopita aliposherehekea ushindi wake wa 95 kwenye mechi za kimataifa wakiwafunga 4-1 Korea ya kusini. Akiwa na miaka 31 'Saint Iker' mtakatifu Iker sasa atakuwa kiomba kuisadia Spain kushinda kombe la tatu kubwa mfululizo - huku mchezaji mwenzake Xavi Hernandez ambaye tayari amecheza mechi 108 tangu acheze mchezo wake wa kwanza miaka 12 iliyopita.
Sweden, Jamhuri ya Ireland na Ukraine nazo zimetoa wachezaji waliocheza mechi zaidi ya 100 katika vikosi vyao, Anders Svensson akiwa anamfuatia Casillas kwa kuichezea Sweden mechi 126, akaifuatiwa na mchezaji mwenzie wa timu taifa Olof Melberg akiwa amecheza mechi 113. Shay Given Given wa Ireland akiwa amecheza mechi 121, Robbie Keane amecheza mechi 116, huku wachezaji wawili wa Ukraine Anatoliy Tymoshchuk akicheza mechi 112, na Andrey Shevchenko 107.
Listi ya wachezaji wazoefu zaidi kwenye UEFA EURO 2012:
Iker Casillas (Spain, 130 caps)
Anders Svensson (Sweden, 126)
Shay Given (Republic of Ireland, 121)
Giorgos Karagounis (Greece, 117)
Miroslav Klose (Germany, 116)
Robbie Keane (Ireland, 116)
Anatoliy Tymoshchuk (Ukraine, 116)
Dennis Rommedahl (Denmark, 116)
Gianluigi Buffon (Italy, 114)
Olof Mellberg (Sweden, 113)
Xavi Hernández (Spain, 108)
Andriy Shevchenko (Ukraine, 107)
Lukas Podolski (Germany, 97)
Damien Duff (Ireland, 96)
Rafael van der Vaart (Netherlands, 96)
Xabi Alonso (Spain, 95)
Josip Šimunić (Croatia, 95)
Ashley Cole (England, 94).
No comments:
Post a Comment