Vikosi vya UEFA EURO 2012 vimeshatajwa, lakini nini unajua kuhusu wachezaji 368 watakaokuwepo kwenye Euro? Nani mrefu? Nani mdogo zaidi? shaffihdauda.com inakupa majibu yote haya.
UREFU
Ujerumani wanaweza kuwa hatari zaidi kwenye mipira ya juu . . . . . . . isipokuwa labda watakapocheza na Croatia. Timu zote mbili zina wastani mzuri wa wachezaji warefu wa sentimita 185, wakati huo mchezaji mrefu zaidi akiwa ni kipa wa Sweden Andreas Isaksson mwenye urefu wa sentimita 199.
MAGOLI
Uholanzi ndio timu iliyofunga mabao mengi zaidi kwenye kufuzu, mabao 37, wakati Ugiriki wakiwa wamefunga mabao 14, huku sita kati ya hayo yakiwa yamefungwa na mabeki.
Klaas Jan Huntelaar, ndio mfungaji mwenye njaa zaidi akiwa amefunga mabao 12, huku Miroslave Klose akiwa wa pili kwa kufunga mabao 9.
UMRI
Italy, Russia, Jamhuri ya Ireland na Sweden ndio watakuwa na wachezaji wakongwe zaidi kwenye michuano hii, wakiwa na wastani wa umri wa miaka 28, huku Ujerumani wakiwa ndio timu yenye wachezaji wadogo zaidi kwenye michuano.
Akiwa na miaka 37, golikipa wa Ugiriki Kostas Chalkias ndio mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi, huku beki wa Uholanzi Jetro Willems akiwa ndio mdogo zaidi akiwa na miaka 18 na ikiwa atapata nafasi ya kucheza atakuwa ndio mchezaji mdogo zaidi kuwahi kucheza kwenye michuano hii.
No comments:
Post a Comment