Michuano ya ulaya bila uwepo wa mchezaji bora wa bara hilo ni jambo ambalo lilianza kuonekana linawezekana baada ya Ureno kutoa suluhu 4-4 na Cyprus kwenye mchezo wao wa kwanza kufuzu, kabla ya kufungwa 1-0 na Norway. Baadae Shirikisho la soka la Ureno likamtimua kazi Carlos Queiroz na kumpa ajira Paulo Bento.
Ingawa ndio kocha mwenye umri mdogo zaidi kwenye Euro akiwa na miaka 42, Bento ameonyesha kwamba hana uoga katika kufanya maamuzi makubwa: ameshamtimua kwenye timu ya taifa Ricardo Carvalho na Jose Bosingwa, huku akipunguza presha kwa Cristiano Ronaldo kwa kumfanya acheze huru kama mshambuliaji kivuli. Jambo hilo liliisaidia Ureno sana kwenye mchezo wa play off dhidi ya Bosnia and Herzegovina.
Bento na Ronaldo walikuwa ni wachezaji wa timu moja pale Sporting Lisbon, na sapoti kubwa aliyoionyesha Ronaldo kwa Bento wakati wa sakata la Carvalho, limeukomaza uhusiano wa wawili hao.
Bento amekuwa na mahusiano mazuri na sana na wachezaji kuliko ilivyokuwa kwa Carlos Queiroz, na ushindi wa 4-0 dhidi ya Spain mwezi November 2010 uliongeza kujiamini ndani ya kikosi. Hilo linadhihirishwa na mfumo wa ongezeko la bonasi wachezaji wa Ureno walivyokubaliana na shirikisho: hawatopata kiasi chochote cha fedha kama watashindwa kuvuka kwenye hatua ya makundi, na kiasi cha kwanza watakipata ikiwa tu watafanikiwa kufika hatua ya robo fainali.
Huku wakiwa na timu mojawapo inayopewa nafasi ya juu kubeba taji Ujerumani, wakipewa nafasi ya kuongoza kundi lao, labda itabidi Ureno wawafunge Denmark na Uholanzi kuweza kufika kwenye hatua ya robo fainali. Ikiwa Ronaldo atacheza kwa mafanikio japo nnusu kama ilivyo kwa Real Madrid basi lolote linawezekana.
WACHEZAJI MUHIMU
Cristiano Ronaldo
Hakuna ubishi wala swali kama Ronaldo ni mchezaji bora wa bara la ulaya, lakini siku zote imekuwa ni vigumu kwake kuileta form yake ya kwenye klabu katika timu ya taifa. Wakati Bento alipopewa ukocha alimrudisha kucheza nafasi yake kutoka pembeni, na kumuondolea mzigo wa kuwa kufunga magoli. Lakini ukiangalia rekodi yake ya kutupia nyavuni katika msimu na Real Madrid, michuano hii ndio nafasi nyingine ya Ronaldo kuweza kuirudisha tuzo ya mchezaji bora wa dunia inayomilikiwa na Lionel Messi.
Luis Nani
Atakuwa na jukumu muhimu katika kikosi cha Ureno: winga mwenye kila sifa ambaye sifa yake kubwa ni pale anapokutana na vita ya one against one na mabeki huku akiweza kufunga kwa mashuti ya mbali tena akipiga kwa miguu yote miwili. Hii itakuwa ni advantage kwake kwamba attention yote itakuwa kwa Ronaldo jambo litakalomfanya acheze bila presha. Baada ya kukosa kombe la dunia kutokana na majeruhi wakati wa mazoezi, Nani sasa yupo na hamu ya kuonyesha kwamba yeye ni mchezaji bora pia.
Pepe
Katika hali ya kutokuwepo kwa Carvalho, safu ya ulinzi ya Ureno inaonekana itakuwa na taabu kidogo, hasa ukizingatia Pepe na patna wake Bruno Alves wamekuwa wakijikuta wakipata kadi za mara kwa mara hata pale ambapo wanaweza kuziepuka. Pepe ndio kiongozi mpya wa safu ya ulinzi, na form yake itakuwa muhimu katika kuhakikisha nyavu za Ureno haziguswi na wapinzani wao wenye washambuliaji hatari.
MASWALI
Je Bento anaweza akaleta mshtuko?
Kocha huyu atayari anajua watu gani wa kuwapanga kwenye safu ya ulinzi na ushambuliaji, lakini nafasi pekee ambayo inamtia mawazo ni kiungo cha ulinzi. Joao Moutinho na Raul Meireles tayari wana nafasi kubwa ya kuanza, lakini Bento na uamuzi wa kufanya kwa kiungo anayecheza chini zaidi. Miguel Veloso amecheza kidogo sana akiwa na Genoa msimu huu huku kiungo aliye kwenye form wa Braga Custodio, hajawahi kuichezea timu ya taifa ingawa yupo kwenye kikosi kwa sasa. Kiungo halisi mkabaji atakayebaki nyuma na kuwaruhusu Moutinho na Meireles wacheze kwa mtindo wa box to box.
Lini Nelson Oliveira atapata nafasi?
Mshambuliaji wa Benfica anaweza akawa na miaka 20 na kucheza mechi moja tu, lakini Oliveira ndio jina kwenye mdomo wa kila mtu. Alikuwa ndio mchezaji wa kwanza kupewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mara tu baada ya timu kuingia kambini, na kama washambuliaji Helder Postiga na Hugo Almeida watashindwa kuonyesha uwezo, Oliveira atakuwa ndio mchezaji washabiki watakayetaka kumuona akichukua nafasi ya kuongoza mashambulizi. Ingawa kwa sasa ataanzia benchi.
Je Ronaldo atamfunika Eusebio?
Ikiwa Ureno watashinda taji la Euro 2012, au kukaribia kufanya hivyo, Cristiano Ronaldo anaweza akaondoa ukungu uliopo kuhusu nani hasa ni mchezaji bora wa muda wote wa Ureno. Kwa sasa, Eusebio bado anaaminika na wengi kama ndio mchezaji bora wa historia ya soka la Ureno, lakini Ronaldo anakaribia tena sana. Ikiwa mchezaji huyu wa Real Madrid ataisadia Ureno kushinda taji la ulaya (ambayo haijawahi kushinda kombe la ulaya wa World Cup) ubishi utakuwa umeisha.
MBINU
Bento anapenda kutumia mfumo wa 4-3-3, lakini timu yake inashambulia zaidi kuliko ilivyokuwa chini ya Queiroz, huku beki wa kushoto Fabio Coentrao akipanda mbele na kushambulia kwa kasi akimruhusu Ronaldo kuingia ndani zaidi. Moutinho na Meireles wakicheza kwa mtindo wa box mpaka box, huku Veloso au labda Custodio wakicheza kama kiungo mlinzi, hivyo kwa mchezo wa kwanza, atleast, Postiga atapata nafasi.

No comments:
Post a Comment