Search This Blog

Monday, April 2, 2012

TENGA AKATAA KUJIUZULU KWA MOHAMED

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amekataa barua ya kuomba kujiuzulu ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ya TFF, Said Mohamed.

Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa klabu ya Azam alimuandikia Rais Tenga barua ya kujiuzulu wadhifa huo akipinga kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Alfred Tibaigana juu ya adhabu zilizotolewa na Kamati ya Ligi kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga.

Rais Tenga amesema alimteua Mohamed katika Kamati hiyo kwa kuzingatia uadilifu wake na uwezo wake katika kuongoza, hivyo amekataa barua hiyo ya kuomba kujiuzulu.

Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Mkutano Mkuu wa TFF, Rais Tenga, Oktoba 28 mwaka jana aliunda Kamati ya Ligi ambayo wajumbe wake wanatoka kwenye klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza.

Wajumbe wa kamati hiyo ni Wallace Karia (Mwenyekiti), Said Mohamed (Makamu Mwenyekiti), Damas Ndumbaro, Steven Mnguto, Geoffrey Nyange, Seif Ahmed, Henry Kabera, ACP Ahmed Msangi, Meja Charles Mbuge na Ahmed Yahya.

WASHABIKI 11,056 WASHUHUDIA COASTAL, YANGA
Washabiki 11,056 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Coastal Union na Yanga lililochezwa juzi (Machi 31 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Viingilio katika pambano hilo vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP, sh. 6,000 jukwaa kuu na sh. 4,000 mzunguko. Mapato yaliyopatikana kwenye pambano hilo ni sh. 61,494,000.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 14,664,927.80 uwanja sh. 4,630,335.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (DRFA) sh. 2,515,494.37.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 4,630,335.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,315,167.97 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 463,033.59.

Nayo mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa Machi 31 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 29,716,000 kutokana na watazamaji 8,167 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo.

Baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni sh. 4,532,949.15, kila timu ilipata sh. 5,031,085.25, Uwanja sh. 1,486,465.08, TFF sh. 1,486,465.08, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,084,600.03, FDF sh. 743,232.54 na BMT sh. 148,646.51.

AZAM, RUVU STARS ZAINGIZA MIL 1.5
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Ruvu Stars lililochezwa jana (Aprili Mosi mwaka huu) Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam limeingiza sh. 1,585,000.

Jumla ya watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 1,000 mzunguko na sh. 5,000 jukwaa kuu ni 1,569.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 283,656, uwanja sh. 57,942, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 117,306.08, TFF sh. 57,942, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 28,971 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 5,794.02.


Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment