Search This Blog

Monday, April 2, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH:-TIMU YA TAIFA YA NGUMI KUKABIDHIWA VIFAA VYA MAZOEZI NA     
               LAPF TAREHE 3/4/2012 SAA 4.00 KATIKA OFISI ZA LAPF MILLENIUM
                TOWER KIJITONYAMA.

Awali ya yote shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) tunatoa shukrani za dhati kwa kwa shirika la LAPF kwa mara nyingine  kukubali kuipatia timu ya Taifa ya ngumi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya maandalizi kushiriki mashindano  ya kufuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Casablanca Morocco Aprili 27/2012 na hatimaye mashindano ya Olimpiki Julai 2012 London Uingereza.
Zoezi hilo litafanyika kesho tarehe 03/14/2012 kuanzia saa 4.00 asubuhi  katika Ofisi za LAPF zilizopo jengo la Millennium Tower Kijitonyama.
Timu ya Taifa ya ngumi ipo kambini Kibaha katika shule ya Filbert Bayi ikiwa na jumla ya wachezaji kumi wa uzito wa kuanzia l/fly hadi super heavy ikiwa na jumla ya makocha watatu na dakitali mmoja.
Wachezaji na makocha waliopo kambini ni:-
  1. John Christian             49KG l/fly
  2. Abdalah Kassim          52 kg fly
  3. Emillian Patrick           56 kg bantam
  4. Denis Martin                60 kg l/weight
  5. Victor Njaiti                 64 kg l/welter
  6. Seleman kidunda          69 kg welter
  7. Mohamed chibumbui    69 kg welter
  8. Mhina Moris                 81 kg l/heavy
  9. Haruna Swanga            91kg   heavy
  10. maximillan Patrick        91+  super heavy
  11. Edward Emanuel           kocha
  12. David Yombayomba      kocha
  13. Remy Ngabo                   kocha
  14. Joseph Magesa               daktari
Wote mnakaribishwa kushuhudia tukio hilo kwa maendeleo ya mchezo wa ngumi

Makore Mashaga
Katibu Mkuu

No comments:

Post a Comment