Mwamuzi wa kati aliyejeruhiwa vibaya usoni na mashabiki katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Polisi Dodoma na Azam ya jijini Dar es Salaam ametibiwa na kuruhusiwa baada ya kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Mwamuzi huyo Martin Sanya alijeruhiwa na mashabiki wanaosadikiwa ni wa timu ya Polisi kwa kinachodaiwa ni kukasirishwa na maamuzi aliyokuwa akitoa katika mechi hiyo.
Kutokana na kipigo hicho mwamuzi huyo aliokolewa na kikosi cha kutuliza ghasia ambao wakisaidiana na polisi walimpeleka mwamuzi huyo Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.
Inadaiwa mwamuzi huyo alipigwa na fimbo usoni na alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alishonwa nyuzi mbili.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (Dorefa),
Abubakari Ibrahim, alisema mwamuzi huyo alijeruhiwa na mashabiki baada ya kuchukizwa na maamuzi yake.
Hata hivyo alisema bado hawana taarifa za mtu au watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kutokana na mashabiki kuwa wengi uwanjani hapo.
Katika mchezo huo timu ya Azam ilishinda kwa bao 1-0, lililofungwa na Aggrey Morris dakika 83.

Tuache unazi kwanini waamuzi wanapochezesha mechi ya azam tu ndo wapigwe,nimatokeo yao mabaya wanayotoa nadhani Azam wameandaliwa na TFF.
ReplyDelete