Giants wawili wa soka barani ulaya watakutana uso kwa uso kesho Jumanne, Bayern Munich wanakutana na Real Madrid katika uwanja wa Allianz Arena mjini Munich katika nusu fainali ya Champions league. Bayern wamekuwa na hawashikiki katika uwanja wao wa nyumbani msimu huu wa Champions league na wamefunga mabao mengi huku wakiweka rekodi kwa kuwatandika 7-0 FC Basel. Huku Real Madrid wakiwa na rekodi ya kutisha nje ya uwanja wao wakishinda mechi zote za ugenini na kutoa droo mmoja tu.
Makocha wote wa timu hiz mbili wana uzoefu mkubwa na hatua hii ya mashindano haya. Jupp Heynckes, ambaye alikuwa manager wa Madrid katika msimu wa 1998 ambao ulimaliza ukame wa makombe nje ya Spain kwa Real Madrid - ukame ambao ulidumu kwa miaka 32. Alishinda kombe la Champions league na kulipeleka Bernabau lakini kwa bahati mbaya alifukuzwa baada ya Real kumaliza katika nafasi ya nne, points 11 nyuma ya mabingwa Barcelona. Jose Mourinho na rekodi zake za champions league ni hatari, aliiongoza Porto kuchukua kombe hilo nchini Ujerumani in 2004, kabla ya kuwa na Inter Milan na kuiongoza timu kuitandika Bayern Munich katika fainali ya Champions league katika uwanja wa Bernebeu.
Real Madrid wanapigana vita mbili kubwa sasa hivi, wakiwa viongozi wa ligi ya nyumbani wakipgana vikali na Barcelona, hukuwakiwa ndani ya hatua ya nusu fainali ya Champions league. Kwa upande wa Bayern Munich kufungwa kwao na Dortmund na droo yao dhidi ya Mainz imewafanya wawe na hali ngumu ya kugombania ubingwa wa Bundesiliga. Huku joto la presha ya mchezo huo likizidi kupanda ebu tujaribu kuangalia vita zitakazotea uwanjani kati ya wachezaji wa Bayern na Real @Allianz Arena.

PHILIP LAHM VS CRISTIANO RONALDO
CR7 amekuwa katika kiwango cha ajabu hivi karibuni huku akifunga magoli ya hatari sana yakiwemo dhidi ya Atletico Madrid na Sporting Gijon. Anaonekana amerudisha uwezo wake wa kupiga vizuri set pieces na anatishia amani kila anapopiga mipira hiyo ya adhabu ndogo. Itakuwa ni changamoto kubwa kwa Phillip Lahm kumzuia Ronaldo na atakuwa na wakati mgumu zaidi kwa sababu Arjen Robben atakuwa akijaribu kusogeza mashambulizi mbele jambo ambalo litamuongezea mzigo Lahm. Lahm alipumzishwa dhidi ya Mainz kwa ajili aweze kuwa vizuri kuweza kupambana Ronaldo.
Lahm amekuwa hayupo vizuri katika siku za hivi karibuni, huku katika mechi dhidi ya Dortmund akionekana kutokucheza vizuri, tofauti na siku za nyuma alipokuwa moja ya wapeleka mshambulizi mbele wa Bayern. Inawezekana aliamua kubaki nyuma kutokana na tishio la mashambulizi la wachezaji wa Dortmund. Atakutana na hali nya namna hiyo kesho dhid ya pace ya Ronaldo na wenzie. Lahm itabidi acheze kwa asilimia 120% ya uwezo wake wote ili kuweza kupambana na Cristiano, na ajaribu kwa kila hali kushirikiana vizuri na Robben ili kuweza kuwarudisha nyuma Madrid na hiyo ndio salama yake dhidi ya Mreno Ronaldo mwenye njaa ya kufunga ndani ya dakika zote 90.
ARJEN ROBBEN VS MARCELO/COENTRAO
The flying dutchman atakutana na mpinzani wake wa jadi mbrazili, ni hii itakuwa vita nyingine muhimu na ambayo itachangamsha sana mechi. Robben atakuwa yupo tayari kuwatoa wasiwasi mashabiki wa Bayern baada ya kuonyesha kiwango kibovu dhidi Dortmund na atakuwa na sababu nyingine zaidi ya kufanya vizuri katika mechi dhidi ya Madrid ili kuwaonyesha viongozi wa klabu hiyo walikosea kumuuza. Marcelo amekuwa akisemwa sana juu ya mbinu zake za kuzuia na amekuwa akionekana ndio njia ya nyepesi ya kupitia katika ukuta wa Madrid.
Ni hatari sana anapokuwa amepanda mbele na uelewano mzuri sana na Ronaldo katika wingi ya kushoto, lakini mara nyingi amekuwa akijisahau na kuacha uwazi wa mashambulizi kupita kwake anapokuwa amepanda mbele, kitu ambacho mara nyingi kimekuwa kikiigharimu Madrid. Ikiwa Mourinho ataamua kuweka ukuta mgumuzaidi basi ni wazi atampanga Coentrao mbele Marcelo, kwa kuwa ndio beki wa kushoto alityefanya vizuri katika mechi za ugenini msimu huu. Ingawa Coentrao bado hajaweza kujijengea nafasi ya kucheza zaidi ya Marcelo, na mfano mzuri aliporonga sana katika Spain Derby, akicheza ovyo katika kuzuia na hakufanya chochote katika kupeleka mashambulizi mbele. Ikiwa atapangwa basi itabidi awe makini sana dhidi ya Robben kwani mholanzi huyo endapo ataachiwa nafasi kubwa, kwa hakika atasababisha madhara katika goli la Madrid. Ni juu ya Marcelo/Coentrao kumzuia kiumbe huyu kuweza kung'ara katika mechi hii. Kombinesheni ya CR7/Marcelo na Robben/Lahm italeta utamu sana katika mechi hii, lakini je ni kambi ipi itamfunika mwenzake.
BASTIAN SCHWEINSTEIGER VS MESUT OZIL
Vita ya katikati ya uwanja katika nafasi ya kiungo zote imekuwa inaamua sana mechi. Mechi hii itakuwaktanisha wajerumani katikati ya uwanja na itakuwa niburudani kuona nani ataibuka mbabe. Mesut Ozil amekuwa katika kiwango cha juu msimu wote huu japokuwa hakucheza vizuri katika baadhi ya mechi. Siku zote amekuwa akifanikiwa kuzifungua safu za ulinzi ngumu kutokana na pasi zake za akili. Schweinsteiger na Xabi Alonso wanacheza role moja katika timu zao na itakuwa ni juu ya mchezaji namba 31 wa Bayern kuamua vita hii iweje. Pia atakuatana na mjerumani mwenzake ambaye yupo kwenye form Sami Khedira.
Schweinsteiger ndio kwanza amerudi kutoka kwenye majeruhi makubwa ya enka katika stage hii muhimu ya msimu wa Bayern na kocha wake Heynckes atakuwa akimuangalia mchezaji wake mahiri wa safu ya kiungo akijaribu kuizuia Madrid. Aliingizwa kama subtitue katika mechi dhidi ya Mainz na akama ilivyotegemewa alionekana kukosa match fitness. Kama atapanga hili linaweza kuleta shida kidogo katika timu yake.
No comments:
Post a Comment