Search This Blog

Friday, April 6, 2012

LIVE MATCH CENTRE: ES SETIF 3 - 1 SIMBA SC FULL TIME - SIMBA WAMEPITAAAAA KWA GOLI LA UGENINI

DK 4 za nyongeza zimemalizika tayari na refa bado hajamaliza mpira

90: Simba wanapata goliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

DK 86: Okwi anapiga shuti la mbali na kipa wa Setif anaokoa kwa ustadi 

DK 81: Setif wanapata faulo nje kidogo ya eneo la penati inaogonga mwamba nje - inakuwa free kick.

DK 75: Setif wanapata free kick na inapigwa kiufundi  na juma kaseja anaiokoa kwa ustaadu mkubwa na inakuwa kona tasa.

DK 70: Mpira umetulia sasa Simba wanacheza na Setif nao likewise. Kwa kifupi ume-balance.

DK 67: Okwi anawatoka mabeki wa Setif na kupiga shuti kali linalotoka nje

DK 65: Setif wanakosa bao la wazi 

DK 60: ES Setif 3-0 Simba

DK 54:  Simba wanaonekna kucheza kwa presha kubwa, hivyo kupoteza mpira mara kwa mara jmbao ambalo linawaongezea kasi Setif.

DK 52: Setif wanapata bao la 3 hapa 

DK 46: Setif wanapata goli la kiutatanishi hapa. ES Setif 2-0 sIMBA

Second Half/Kipindi cha pili kinaanza

DK 45: Mpira ni mapumziko

DK 43: Setif wanakosa bao la wazi hapa, Juma Kaseja anaokoa

DK 38: Mwinyi Kazimoto anapata majeraha na natolewa nje kwa machela, pia tayari ameshapata kadi ya njano

DK 35: Setif wanapata bao hapa, walitumia vizuri free kick waliyopata ambayo ilipigwa na kuwapita mabeki wa simba kisha kumfungua mfungaji aliypiga na kutinga nyavuni.

DK 30: Mpira bado 0-0 

DK 25: ES Setif wanashambulia sana goli la Simba lakini bado hawajatengeza hata nafasi moja ya wazi.

DK 15: Dakika inakwenda ya 20 na matokeo bado 0-0. Simba wanaonekana kutulia na ku-handle vizuri mashambulizi ya Setif japokuwa wapo wachache uwanjani.


DK 10: Juma Nyosso wa Simba anapewa kadi nyekundu baada ya kutaka kumpiga ngumi mchezaji wa Setif kwa bahati mbaya refa hakuona lakini mwamuzi wa pembeni aliona hivyo akamuita refa na kumuelezea tukio lilivyokuwa na hatimaye refa akaamua kumtoa kwa kadi nyekundu beki huyu wa simba

DK 5: Mpira ume-balance japo Setif  walianza kwa kasi kushambulia lango la Simba.

DK 1: Kick Off

Zikiwa zimebakia takribani dakika 10 timu zinarudi ndani kujiandaa na mechi.

Timu zimeshaingia uwanjani na sasa kila timu inachukua upande wake na kuanza kufanya warm up.

Takribani dakika 40 kabla ya mpira kuanza kati ya ES Setif ya Algeria na Simba ya Tanzania. Hali ya hewa ni ya kawaida japo kuna baridi na mashabiki wapo wengi hapa uwanjani japo uwanja haujajaa, lakini bado wananendelea kuingia uwanjani. Pia kuna mashabiki takribani 200 wa kitanzania wanaoipa sapoti ya kutosha Simba.

Kikosi cha Simba kinachoanza ni kama ifuatavyo:
MFUMO: 4:4:2

GK
Juma Kaseja,

MABEKI
Shomari Kapombe, Amir Maftah,Juma Nyoso,Kelvi Yondani,

VIUNGO
Patrick Mafisango,Salum Machaku,Mwinyi Kazimoto,Emanuel Okwi

WASHAMBULIAJI

Felix Sunzu,Haruna Moshi

Sub:Ally Mustafa 'Barthez', Nassoro Masoud Chollo, Obadia Mungusa, Victor Costa, Uhuru Seleman, Jonas Mkude na Gervais Kago. Simba itavaa nyekundu juu, bukta nyeupe na soksi nyekundu

16 comments:

  1. All da best smba. Endlea k2pa mambo kaka shaffih atleast kla baada ya dk 5

    ReplyDelete
  2. Tunaiombea simba ushindi wajitahidi kushambulia wasijihami

    ReplyDelete
  3. wachezaji wetu wamekosa nidham ugenini haina haja kumtishia kumpiga mchezaji mwenzako ahhh kaicost team kiac kikubwa mno.

    ReplyDelete
  4. Poleni sana Simba,welcom bak to the VPL

    ReplyDelete
  5. Kaka shaffih nguvu zimeniishia kabisa

    ReplyDelete
  6. Siamaini kama tunaaga mashindano leo, sijui soka letu lini litaonekana kimataifa koz hatufiki mbali kila mashindano.

    ReplyDelete
  7. Wa msimbazi tunaona utaaaaaaaaaamu

    ReplyDelete
  8. hongera sana simba ....well done

    ReplyDelete
  9. Simba wacheka kama kibelala mmhh.......ahhhh,mmmh.....,weekend yetu itakuwaje heeee,mwanamzimbazi.

    ReplyDelete
  10. Okwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  11. Hakika pasaka itakuwa njema MSIMBAZI ketu sijui mabondia wa Jangwani wanajisikiaje

    ReplyDelete
  12. innocent toa comment yako tena,wasiofika mbali ni yanga au maarufu kwa jina la kandambili lakini simba tuko juu!

    ReplyDelete
  13. hivi huwezi kuandika bila kulazimisha maneno ya kingereeza bila sababu

    ReplyDelete
  14. hivi wachezaji wa kibongo wana matatizo gani au toka wachezaji wa yanga walivyompiga refa imekuwa style... mimi nadhani bila Nyoso kufanya upuuzi ushinda ungekuwa mapema,kama ningekuwa kiongozi simba ningempa Nyoso adhabu ili iwe fundisho......... hongera msimbazi

    ReplyDelete