Search This Blog

Monday, April 16, 2012

CHELSEA KIBOKO YA BARCELONA: BARCA HAWAJAWAFUNGA CHELSEA TANGU MWAKA 2006

Pamoja na mafanikio yote waliyonayo, kuzifunga timu tofauti rekodi ya Barca dhidi ya Cheslea sio nzuri. Ukiachana na ushindi wa goli la kitatanishi la Andres Iniesta katika nusu fainali ya champions league mwaka 2009, Barcelona hawajawafunga Chelsea katika mechi za mwisho zilizopita - mara ya mwisho kuwafunga ilikuwa mwaka 2006.

HAYA NI BAADHI YA MATOKEO YA MECHI CHELSEA KATIKA MIAKA 5 ILIYOPITA UKIUTOA MCHEZO WA MWISHO WA CHAMPIONS LEAGUE.

DRAW. FC Barcelona-Chelsea (1-1, March 8th, 2006). Ronaldinho na lampard wote wanafunga magoli kati mechi. Huu ndio mwaka Barcelona walienda kuchukua ubingwa wao wa pili wa Champions league kwa kuwafunga Arsenal katika fainali mjini Paris.

DEFEAT. Chelsea-FC Barcelona (1-0, October 18th, 2006).
Katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa ulaya. Drogba aliupiga msumari pekee uliofunika jeneza la mechi hii.

DRAW. FC Barcelona-Chelsea (2-2, October 31st, 2006).
Mechi ya pili ya hatua ya makundi. Mechi iliishia kwa sare ya 2-2 shukrani zimuendee Frank Lampard kwa kuioka timu yake dakika za mwisho za mchezo.Chelsea walimaliza nafasi ya kwanza kwenye group na Barcelona wakawa wa pili.

DRAW. FC Barcelona-Chelsea (0-0, April 28th, 2009).
Ulikuwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya katika uwanja wa Nou Camp na mechi ikaishia kwa sare pacha.

DRAW. Chelsea-FC Barcelona (1-1, May 6th, 2009).  Essien alianza kufunga goli nakuwapa uongozi the blues, lakini baadae katika dakika za mwisho kabisa ya mchezo Andres Iniesta aliwapeleka Barca fainali ya Champions league huku wakiwa pungufu uwanjani baada ya Eric Abidal kutolewa nje kwa red card. Barca walienda fainali nakwenda kuwafunga Man United 2-0 nakubeba ndoo mjini Rome Italia.

No comments:

Post a Comment