Search This Blog

Tuesday, March 20, 2012

SIMBA NA MTIBWA SUGAR ZAINGIZA MIL.31 UWANJA WA JAMHURI

Mechi namba 146 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na Simba iliyochezwa Machi 18 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro imeingiza sh. 31,230,000.
 
Jumla ya watazamaji 10,410 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000. Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,763,898.31 kila timu ilipata sh. 6,508,230.51, uwanja sh. 2,169,410.17.
 
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) sh. 867,764.07, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,169,410.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,084,705.08, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 216,941.02 na asilimia 10 ya gharama za mechi sh. 2,169,410.17.
 
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi sh. 120,000 na tiketi sh. 2,480,000.
 
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 728,700 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kilipata sh. 624,600.

No comments:

Post a Comment