Search This Blog

Tuesday, March 20, 2012

LIONEL MESSI AONGOZA KWA UTAJIRI KWENYE SOKA - AMFUNIKA RONALDO NA BECKHAM

Kwa mara nyingine tena Lionel Messi anatengeza kichwa cha habari, Messi ndio mwanasoka anayelipwa mkwanja mrefu kuliko wote duniani, huku David Beckham akishika nafasi ya pili na Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya tatu.

Kutokana na ripoti iliyotolewa na jarida la France Football, ambayo imetoka leo, mshambuliaji huyo wa Barcelona anaingiza €33million kwa mwaka kupitia mishahara na fedha za matangazo.

LA Galaxy midfielder na mchezaji wa zamani wa Manchester United Beckham, ambaye amekuwa akiongoza kwa muda mrefu listi hii, amekuwa wa pili akiingiza €31.5m, wakati star wa Real Madrid Ronaldo akikusanya €29.2m ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Samuel Eto'o nae yupo katika nafasi ya nne akiingiza €23.3m, huku Wayne Rooney akikamata nafasi ya tano na €20.6m.

Wengine ni kama wanavyoonekana hapo chini kwenye listi.

MESSI AZIDI KUFUNIKA.
173903_hp.jpg
Lionel Messi (Barcelona)
David Beckham (LA Galaxy)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Samuel Eto'o (Anzhi)
Wayne Rooney (Man United)
Sergio Aguero (Man City)
Yaya Toure (Man City)
Fernando Torres (Chelsea)
Kaka (Real Madrid)
Philipp Lahm (Bayern Munich)
€33m
€31.5m
€29.2m
€23.3m
€20.6m
€18.8m
€17.6m
€16.7m
€15.5m
€14.3m

No comments:

Post a Comment