Nikiwa mpenzi mkubwa wa mpira wa miguu,nimelazimika kuandika waraka huu kwako juu ya sakata ya ligi ya taifa mkoa wa Tanga,kufuatia kuibuka malumbano juu ya michezo ya mwisho inazozihusu AFRICAN SPORTS na SMALL PRISON...Taarifa iliyotumwa jana katika kipindi cha michezo extra haikua na ukweli halisi wa sakata lenyewe,bali ilikua na nia ya kuipaka matope A SPORTS na kuficha ukweli ulivyo.
Uchunguzi niliyoufanya nimegundua ya kwamba SPORTS na PRISON zote zilicheza mechi 3 na zikawa zimelingana point zote zikawa na point 5 na uwiano wa magoli ukiwa sawa na zikiwa zimebakisha mechi 1 dhidii ya timu 1 ya SEGERA UNITED.
Sasa kilichotokea SMALL PRISON walitangulia kucheza mechi yao ya mwisho na SEGERA wakishinda magoli 5 kwa 1 ,huku mechi ikigubikwa na shutuma za upangaji wa matokeo..
Baada ya mechi hiyo ikafuata mechi ya mwisho ya SPORTS dhidi ya haohao SEGERA na SPORTS ikihitajika kushinda magoli 5 kwa 0 ili iwazidi PRISON na kupata nafasi .Hadi dkk 34 ya mchezo huo SPORTS walikua mbele kwa magoli 3 kwa 0,ikionekana dhahiri wametumwa kuitibulia SPORTS ,waligoma kuendelea na mchezo ..Ili kuwanyima SPORTS nafasi ya kuongeza magoli zaidi.
HITIMISHO; Naomba museme ukweli SPORTS na PRISON ni timu gani ilitengeneza mazingira ya rushwa na kubebwa?.Ikiwa SPORTS iliingia uwanjani kucheza mechi ya mwisho pasipo na kuinunua mechi hiyo ,inakuaje mnaibeza eti inabebwa!!Nadhani waraka wa jana tar 19 uliotumwa kwenu haukuwa na ukweli wowote kwa maoni yangu binafsi.
wako mpenda soka nikiwa Tanga,NURU JUMBE.
No comments:
Post a Comment