David De Gea amekuwa na wakati mgumu sana katika msimu wake wa kwanza kwenye timu yake Manchester United. Tangu mchezo wake wa kwanza ambapo United waliwafunga wapinzani wao Manchester City mapungufu yake yalionekana na ilikuwa dhahiri kuwa angepata wakati mgumu kuzoea soka la England.
Vyombo vya habari na mashabiki walikuwa wepesi kumhesabia kila kosa alilofanya. Kumbukumbu za wengi zilirejeshwa kwenye jinsi United ilivyochukua miaka mitatu kumpata mrithi sahihi wa Peter Schemeichel ambaye alikuwa Edwin Van Der Sar na wengine walimfananisha De gea na baadhi ya makipa wabovu waliowahi kupita Old Trafford kama Masimmo Taibi na Ricardo.
Tetesi zinasema kuwa Sir Alex Fergusson alikuwa na majina matatu ya warithi wa Edwin Van Der Saar, Manuel Neur, Marten Stekelenburg na De Ge . Neuer alichagua kwenda Bayern Munich, Sir Alex alikuwa anataka kipa mwenye umri mdogo hivyo akamchagua De Gea mwenye miaka 22 badala ya Stekelenburg mwenye miaka 29, kocha wa makipa wa United Eric Steele alikuwa na uhakika kuwa bosi wake amefanya uchaguzi sahihi, lakini mwanzo wake kwenye maisha ya soka la England ulikuwa mgumu na baadhi ya mashabiki walianza kupata wasiwasi na uamuzi wa kocha wao.
Steele alisafiri mara kadhaa kwenda sehemu mbalimbali kutazama michezo ya Atletico Madrid msimu uliopita kuangalia maendeleo ya De Gea, alienda mbali zaidi na kuanza kujifunza lugha ya kihispania ili mawasiliano kati yao yawe rahisi wakati atakapoanza kuichezea United .
De Gea amekuwa akifanya makosa yake na mengi kati ya hayo yamekuwa kushindwa kuzoea mapema soka la Uingereza ambalo ni tofauti kabisa na soka la Hispania alikotokea De Gea lakini hakuna ubishi juu ya kipaji alichonacho kijana huyu na kwa umri wake ana uwezo mkubwa wa kupiga hatua na kuwa mlinda mlango bora duniani kama ilivyokuwa kwa mhispania mwenzie Iker Casillas.
Presha ya fedha nyingi zilizotumika kumsajili (paundi milioni 18) inaonekana kumuelemea wakati mwingine na taratibu amekuwa akiizoea hali halisi ya soka la England.
Wakati anafika England De Gea alikuwa hajawahi kuichezea timu yake ya Hispania ambako kwa sasa yeye ni kipa wa nne kwa ubora nyuma ya Casillas, Reina, na Victor Valdez lakini uzoefu wa ligi alikuwa nao kwani alikuwa amecheza michezo 84 ya ligi ya Hispania akiwa na Atletico Madrid pamoja na kuwa na umri mdogo, ukiachilia mbali michezo 84 ya ligi, De Gea ameiwakilisha timu yake ya taifa ya vijana mara 61 huku akiwa na taji la ubingwa wa ulaya.
Tangu alipoumia Anders Lindergaard, De Gea amerejesha imani ya mashabiki wa United kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha. Ukifuatilia kwa ukaribu michezo miwili ambayo United ilifungwa na Athletic Bilbao utagundua kuwa kama isingekuwa uwezo mkubwa wa De Gea wa kuokoa mabao ya wazi huenda United ingefungwa mabao zaidi ya matano waliyofungwa kwenye michezo miwili. Rudi kwenye mchezo wa ligi kuu ya England ambao Man United ilitoka sare na Chelsea na hapo utaona jinsi De Gea alivyoiokoa timu yake kupata pointi muhimu kwenye matokeo ya sare ya mabao matatu .
Bado anahitaji kujenga mwili zaidi ili awe na uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya timu kama Stoke City ambazo zinacheza soka la nguvu sana lakini umbile lake jembemba linamsaidia kuwa na wepesi wa kuruka na kuokoa mashuti ambayo wengi hutegemea kuyaona yakiishia wavuni.
Moja ya sababu ambazo zimeisaidia United kukalia kiti cha uongozi wa EPL ni uwezo wa De Gea ambao ameuonyesha wakati huu ambapo ligi inaelekea ukingoni.
haaa haaa haaa,atlast Degea kawanyamazisha waingereza,waliacha kuzungumzia maflop wao kina caroll na makinda wao ambao hawana vipaji kivile ila wako over rated,keep on Degea kalisha watu kimya
ReplyDeleteKimya sasa anawafunga mdomo na anachukua ubingwa kwa mara ya kwanza na kuwashnda hao wanaomsema vbaya.
ReplyDelete