Ni Chelsea timu ambayo nilipata mafanikio makubwa katika career yangu ya soka, dhidi ya Napoli ambayo ilinipa nafasi kubwa ya kwanza na kunifanya kuwa mzuri kama ambavyo nilikuwa.
Hivi ni vitu viwili ambavyo nitashukuru milele na nitakuwa pale San Paolo nikiangalia mechi ambayo nitakuwa na hisia za mchanganyiko.
Naples ni mji mzuri, wenye watu wazuri na wenye vipaji, pia ni mji wenye matatizo ya kijamii lakini wanapenda sana football.
Nilikuwa na bahati kucheza pale katika wakati bora zaidi wa maisha yangu ndani ya klabu ile na nimekuwa nikijisikia vizuri kwa kuweza kucheza mahala pale.
Kwa Napoli kurudi katika Champions league, wakiingia katika hatua ya mbele zaidi, kunamaanisha vitu vingi sana kwa mashabiki na wanastahili kuwepo pale kwasababu wanaishi kwa ajili ya soka.
Wachezaji wakiwa wanafanya mazoezi katika shimo la Simba - Uwanja wa Napoli. |
Huu utakuwa mchezo mzuri sana wenye kuvutia na matokeo sitaki kutabiri. Kitu ninachoweza kusema patawaka moto mahala pale.Ile ni sehemu maalum na muda mwingine unaingia uwanjani na unahisi kama kunachemka. Ni hisia nzuri sana, unahisi kama wewe ni Simba. Itakuwa hivyo dhdi ya Chelsea.
Upendo wa mashabiki wa Napoli unaleta mwamko mkubwa kwa wachezaji na kuwatia nguvu. Nilikuwa pale kipindi Maradona aliporudi kwa mara ya kwanza (Ciro Ferrara testimonial in2005) ilikuwa hatari.
Inabidi uelewe nini Maradona anamaanisha kwa watu wa Naples. Anaheshimika na kupendwa kuliko, nan i kitu kimoja wapo ambacho kinaufanya mchezo wa soka kupendwa.
No comments:
Post a Comment