Central midfielder wa Yanga natimu ya taifa ya Rwanda Amavubi, Haruna Niyonzima 'Fabregas', amefunga mjadala wa mechi yao dhidi ya Zamalek ya Misri na kusema imebaki historia na sasa wanajiandaa kwa ajili ya kufanya maajabu mechi ya marudiano nchini Misri.
Mnyarwanda huyo aling'ara kwenye pambano la kwanza lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Akizungumza jana, Fabregas alisema kwa sababu mechi imeshapita na wao "Hatutaki kujutia, mechi imeshapita sasa ni historia, ninachowaambia mashabiki, watulie kwa sababu hiyo. Sasa tunaganga kwa ajili ya mechi inayofuata," alieleza Fabregas.
"Tuna nafasi ya kujiandaa kabla ya mechi hiyo na naamini tutafanya vizuri. Tunakwenda tukijua tuna deni tuliloshindwa kulitimiza kwenye uwanja wa nyumbani."
Katika mchezo huo, Yanga ingeweza kuibuka na ushindi mnono kama wangetumia vizuri nafasi nyingi za wazi kufunga zilizopotezwa na washambuliaji Devis Mwape na Kenneth Asamoah.
Kocha msaidizi wa Zamalek, Esmail Yossef amesifu uwezo wa nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa kuwa makini nao katika mechi ya marudiano.
............................................................................
Wakati huo huo kocha wa Yanga, Kostadin Papic ameshangazwa na vitendo vyasivyo vya kizalendo vya mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia Zamalek ya Misri akisema hajawahi kuona.
Papic alisema ni kitu cha kushangaza, kutokana na idadi kubwa ya mashabiki kuishangilia Zamalek.
"Sikutegemea kitu kama hicho kama kinaweza kutokea hapa, yaani Zamalek walipata mashabiki wengi wa kushangilia kiasi kile, sijawahi kuona," alisema Papic.
Kauli ya Papic ilipokewa na kocha msaidizi wa Zamalek, Esmail Yossef aliyewashukuru mashabiki wa klabu ya Simba na kusema: "Tunawashukuru kwa kutushangilia kwani hatukutegemea hilo."
Hata hivyo, mashabiki wa Simba walivyofanya ni kama wamelipiza kisasi kutoka kwa wapinzani wao wa jadi Yanga kuishangilia TP Mazembe ilipocheza na Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.
No comments:
Post a Comment