Search This Blog

Monday, January 9, 2012

PAPIC: TUMECHEZA CHINI KIWANGO MAPINDUZI CUP


Head coach wa Yanga, Konstadin Papic amesema hakuridhishwa na kiwango kibovu kilichooneshwa na wachezaji wake katika mechi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan juzi usiku.

Katika mechi hiyo, Yanga ilifungwa mabao 3-0 na kuaga michuano hiyo.

Akizungumza mjini hapa jana, Papic alisema kuwa mbali ya wachezaji hao kuonesha kiwango cha chini lakini waliweza kuchanganyikiwa baada ya Azam FC kupewa penati katika dakika za mwanzo za mchezo huo.

“Kiwango chao sikuridhika nacho lakini bao la kwanza liliwaathiri wachezaji wangu”, alisema.

Matokeo hayo yaliiwezesha Azam kutinga hatua ya nusu fainali za michuano hiyo huku Yanga ikifungasha virago baada ya kumaliza mechi zake za makundi ikiwa na pointi 3.

Katika mchezo huo, Yanga walionekana kuzidiwa kwa kila idara kutokana na kiwango dhaifu walichoendelea kukionesha tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Azam FC ambayo ilionekana kuukamia mchezo huo iliandika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati lililofungwa na John Boko katika dakika ya tano baada ya Mohammed Mbegu kumchezea vibaya mshambuliaji wa Azam FC.

Kipre Tchetche ndiye aliyekuwa mwiba mchungu kwa Yanga baada ya kufunga mabao mawili katika dakika ya 29.


1 comment:

  1. Tia tia maji Zamaleck hii hapa tumecheza chini ya kiwango! Yanga wanahitaji kumaliza matatizo ya kiutawala ili kuweza kujenga timu ya ushindani la sivyo hadithi itakuwa hiyo hiyo siku zote! Players have no morale!!!

    ReplyDelete