Search This Blog
Monday, January 9, 2012
NEIL WARNOCK ATIMULIWA QPR - MARK HUGHES NJIANI KUCHUKUA KIBARUA.
Kocha wa zamani wa Fulham na Manchester City, Mark Hughes, anatarajiwa kujiunga kuifundisha Queens Park Rangers (QPR) baada ya club hiyo ya west London kutangaza kwamba kocha wake Neil Warnock ametemwa kibarua.Club hiyo ilitoa statement kwamba Warnock alijiunga nayo March 2010, ambapo katika michezo 84 klabu iliyocheza chini yake, alishinda 33, draw 27 na kufungwa mara 24. Hiyo statement imesema pia kwamba kocha wake msaidizi Mick Jones na first-team coach, Keith Curle wameondoka, ambapo mwenyekiti wa QPR, Tony Fernandes amesema hayo maamuzi yamefanywa kwa maslahi ya club. Kocha Wanork amesema hajafurahishwa na hatua hiyo, lakini anaiacha club hiyo akijivunia alipoitoa, na kusisitiza kwamba alienjoy kufanya kazi nayo kuliko club yoyote nyingine na kuongeza kuwa “najuta kwa sababu mafanikio hayakuanza kuonekana mapema, kwa sababu yangenipa nafasi nyingine zaidi za mafanikio.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huyu mzee nafurahi kwa kutimuliwa kwake.Ni mbaguzi sana na ameonyesha udhaifu katika kufanya maamuzi.
ReplyDeletewakati QPR wakipanda daraja,Captain alikuwa Adel Taarabt,lkn alipomsajili toto tundu Balton akamtosa Adel...sasa na yeye katoswa.
Anastahili kutimuliwa na ndo maana huwa hadumu kwenye ligi kuu ya England,yy za kwake ni huko chini,madaraja ya chini.
Akafie mbali