Mtoto wa kiume wa Romario amesifiwa kama mmoja ya wachezaji makinda wanafuata nyayo za El phenomena Ronaldo baada ya kufunga goli katika michuano mikubwa kabisa ya vijana nchini Brazil.
Romarinho, 18, aliingia akitokea benchi na kufunga bao la ushindi kwa timu yake ya Vasco Da Gama katika ushindi wa 3-2 dhidi ya San Fransico.
Mkongwe Ronaldo, ambaye alikuwa mmoja wa watazamaji wa mchezo huo alisema kupitia mtandao wa twitter kwamba kijana huyo mtoto wa Romario ana vinasaba vya ustaa.
“Hili goli lilikuwa katika style ya Baba: alisema Romarinho. “ Nina bahati kuwa karibu yake kwa masaa 24 kila siku. Nimejifunza vitu ninapokuwa nae, na hata goli nililofunga nikiwa katikati ya walinzi ni mbinu nilizofundishwa na Baba.”
Kijana huyo ambaye anacheza zaidi kama kiungo mshambuliaji amekuwa akicheza kwa presha kutokana na watu kumfananisha na baba yake, “ Presha ni kitu cha kawaida katika soka, lakini ni mbaya zaidi kwangu kwakuwa ni mtoto wa Romario.
MWANGALIE ROMARINHO AKIFUNGA BAO LA 3 NA LA SUHINDI KWA VASCO DA GAMA
Affirmative!!!!!!!!!
ReplyDelete