BAADA ya harakati za muda mrefu, Simba imenasa kifaa cha timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, ambacho kilitwaa Kombe la Chalenji wikiendi iliyopita.
Simba kwa miaka miwili ilikuwa ikimfukuzia beki wa kushoto, Godfrey Walusimbi na sasa kazi hiyo imefikia tamati.
Walusimbi mwenyewe amethibitisha kuwa atajiunga na Simba kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ujio wa Walusimbi, ambaye anahesabiwa miongoni mwa mabeki bora wa kushoto katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni wazi utawapa presha mabeki wa sasa wa timu hiyo, Amir Maftah na Juma Jabu, ambao wamekuwa
wakipokezana nafasi hiyo katika kikosi hicho cha Msimbazi.
Maftah ni majeruhi kwa muda mrefu, sasa Jabu anatamba kwenye nafasi hiyo.
Walusimbi sasa ameamua kujiunga na Simba baada ya kufanya majaribio katika nchi za Sudan na Ethiopia.
Baada ya kukwama kupata timu huko, alirudi Uganda na kujiunga na Bunamwaya, ambako mkataba wake unamalizika baada ya miezi mitatu.
Simba walicheza karata yao wakati wa Kombe la Chalenji na kumshawishi Walusimbi kujiunga nao.
Walusimbi ambaye alicheza mechi zote za Chalenji akiwa amevaa jezi namba 15, alisema; Naipenda Simba na ndiyo klabu yangu ninayokuja kuichezea msimu ujao.
Nimeshafanya mazungumzo na viongozi wao ninachosubiri ni kumalizia mkataba wangu na Bunamwaya na baada ya hapo, nitakuwa huru kukamilisha mambo yangu,alisema Walusimbi, ambaye jana Jumatatu aliondoka na The Cranes kurudi kwao Uganda.
Search This Blog
Tuesday, December 13, 2011
HATIMAYE WALUSIMBI KUJIUNGA NA SIMBA MSIMU UJAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment