Search This Blog

Tuesday, December 13, 2011

PAMOJA NA KUWA NA MATOKEO MABAYA-BIDHAA MAN UNITED ZAENDELEA KUFANYA VIZURI SOKONI


Pamoja na kwamba club ya soka ya Manchester United imeshuka kutoka nafasi ya kwanza na kuwa ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa kwa kipindi cha miezi miwili na kutolewa katika ligi ya mabingwa wa ulaya, lakini bado bei za bidhaa za club hiyo ziko pale pale na nyingine zimeongezeka.

Bidhaa kubwa ya man u ambayo inauzwa kwenye maduka mengi Dar es salaam ni jezi, na bei zake zinafanana kwa asilimia kubwa, sasa hivi jezi ya Man U inauzwa elfu 35 kutoka elfu 30 miezi miwili iliyopita, ambapo jezi ya Man U ndio inayoongoza kwa kuuza.

Ni utafiti mdogo uliofanywa na Millard Ayo kujaribu kuangalia kama kushuka kwa Man U kumeathiri mauzo ya bidhaa zake madukani, japo ligi kuu ya England haijamalizika, bado round ya kwanza ambayo kila timu inacheza michezo 19 haijamalizika.

Man U katika miezi miwili iliyopita wamekuwa na matokeo mabovu mpaka kupelekea kutolewa kwenye kombe la FA,Ligi ya mabingwa pamoja na kupata wachezaji majeruhi.

Nimegundua sio jezi za Man U peke yake zilizopanda bei DAR ES SALAAM, hata gum ambazo huwa anazitafuna sana kocha Alex Ferguson nazo zimepanda bei, zinaitwa TREDENT ambazo kutoka shilingi elfu 3 miezi miwili iliyopita, wanaozitumia wameongezeka, ambako kwenye duka wanakoziuza, wanasema kwa siku wanaweza kumaliza box moja, ambapo mwanzo zilianza kwa kuuzwa kwa shilingi 2500.

No comments:

Post a Comment